SI KWELI Je, asali ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari kama mbadala wa sukari?

SI KWELI Je, asali ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari kama mbadala wa sukari?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kuna dhana inayosambaa kuwa asali ni salama zaidi kuliko sukari kwa sababu eti ni ya asili especially kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.

Lakini je, kuwa na asili ya asali kunamaanisha kuwa haina madhara kwa kiwango cha sukari kwenye damu?

ASALI JF.png
 
Tunachokijua
KumeKuwepo na nadharia inayodai kuwa matumizi ya asali ni bora zaidi kuliko Asali hasa kwa watu ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari.

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Asali haipaswa kutumika ama hakuna faida ya kuitumia kama mbadala wa sukari kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.

Aidha JamiiCheck imefanya mahojiano na Dkt. Gregory Mkalawa kutoka Tabora, ambaye amefafanua kuwa Asali na Sukari kavu zote zinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu.

Ingawa kwa kawaida kueleza kuwa asali inaweza kuwa na faida zaidi kuliko sukari ya kawaida. Lakini kwa mtu mwenye kisukari, asali haipaswi kutumika kama mbadala wa sukari.

Ameongezea kuwa asali ina mchanganyiko wa glucose, fructose, na kiwango cha madini pamoja na antioxidants. Ukilinganisha na sukari ya kawaida ambayo yenyewe ina sucrose peke yake.

Pamoja na hayo, kiwango cha sukari yenyewe kwenye asali ni kikubwa zaidi ukilinganisha na sukari ile ya kawaida.

Kwa hiyo ndio maana tunasema matumizi ya asali hayapaswi kuwa mbadala wa sukari ya kawaida kwa mtu ambaye ana shida hii ya kisukari
Back
Top Bottom