Ila pia wapo wanyamwezi waliochanganyika kuoana na kuzaa na washirazi ambapo kizazi chao wanajiita waafro shirazi.
Hapa ngoja nikueleweshe kidogo.
Mzanzibar akija bara imeshazoeleka kuonekana kama hana kabila, lakini ukweli ni kuwa wengi wa wazanzibari ni wahadimu na wengine ni waafro shirazi kwa maana ni mulato (Afrika na shirazi) na wengine makabila yao yamestik kuwa vile vile kwakuwa hawakuwa na muingiliano wa mahusiano ya moja kwa moja na washirazi.
Moja ya makabila hayo ni yale ambayo walikuwa wakichukuliwa bara na kupelekwa visiwani kama watumwa enzi za biashara hiyo (Kamsome Tip-Tippu) na wengine ni wale ambao walitoroka bara kuepuka kuchukuliwa watumwa na kukimbilia visiwani kwa wakati huo.
Washirazi waizaa sana na wahadimu kuliko haya makabila yaliopelekwa visiwani enzi za utumwa na ndio maana wengi wa waafro shirazi sio kutoka katika haya makabila mengine.