Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Kwa taarifa yao Asili ya Neno Afro Shirazi ni muunganiko wa vyama 2 vya siasa huko visiwani navyo ni AFRICAN PARTY NA SHIRAZ PARTY. Viongozi wa vyama hivyo waliona ni busara kuunganisha nguvu pamoja na wananchi kwa kuungana pamoja na chama cha AFRO SHIRAZ PARTY kiliundwa chama hiki ndiyo kilichosimamia mapinduzi ya znz na baadaye kuungana na TANU ambapo sasa ni Chama Cha Mapinduzi
African Association na Shiraz Association, mkuu
 
Sawa. Je asili yako ni wapi?
Ingia kwenye [emoji116][emoji116][emoji116]huu uzi

Sent from my Infinix X573 using JamiiForums mobile app
Mafia
 
Sababu ya Waajemi (Wairani) kuhamia Afrika Mashariki


Msomi huyo ni mjumbe wa Kituo cha Utafiti cha Shrika la Utamaduni na Utalii la Iran ambaye hivi karibuni ametembelea Kenya na Tanzania kwa ajili ya kutayarisha orodha ya kitaalamu ya athari za kongwe za Kiirani katika nchi hizo. Katika mahojiano na IQNA, ameashiria historia ya Wairani na Waislamu wa madhehebu ya Shia Afrika Mashariki na kusema: "Kwa mujibu wa nyaraka na ushahidi wa kihistoria, Ushia (Madhehebu ya Ahul Bayt wa Mtume SAW) uliingia katika visiwa vya Zanzibar na Tanganyika zaidi takribani miaka 1000 iliyopita." Anaongeza kuwa Pwani ya Afrika Mashariki kwa muda wa mamia ya miaka imekuwa mwenyeji wa wahajiri na watalii kutoka nchi na mataifa mbali mbali kama vile Waarabu, Wairani, Wachina na Waasyria n.k.

Ridhwanifar anaongeza kuwa: "Katika karne ya nane Miladia (CE) sawa na karne za awali za Hijria Qamaria, Waaarabu walianza hatua kwa hatua kugura kutoka kwao na kuweka makao mapya katika pwani ya Afrika Mashariki hasa Zanzibar ambapo walikuja na bidhaa nyingi za matumizi kama vile vikombo, sabuni, vioo vya rangi na kuwauzia wenyeji wa eneo hilo mkabala wa kupokea bidhaa za kilimo.

Kuingia Washirazi Afrika Mashariki na kuunda utawala Zanzibar

Ridhwanifar anasema wakati Waajemi (Wairani) walipowasili katika pwani ya Afrika Mashariki takribani miaka 1000 iliyopita waliunda utawala wao ambao makao yake makuu yalikuwa Zanzibar. Washirazi ndio wahajiri pekee walioingia Afrika Mashariki kwa nidhamu maalumu kwani waliweza kujumuika na wenyeji wa eneo hilo kiutumaudni na kijami. Maingiliano hayo baina ya wahajiri kutoka Shiraz nchini Iran na wenyeji wa Afrika Mashariki ndio chanzo cha kuibuka ustaarabu wa Kiswahili na lugha Kiswahili.

Msomi huyo kutoka Iran anasema: "Nyaraka za kihisotria zenye kuaminika zimeandikwa kuwa, 'katika karne za nane na tisa miladia, mfanyabiashara (Amir Al-Hassan )kutoka Shiraz huko Uajemi (Iran) akiwa na wanae saba wakiwa katika meli saba walitia nanga katika maeneo ya Lamu, Pemba, Malindi, Mombasa, Kilwa, Unguja na Ngazija na wakaanza kufanya biashara ya dhahabu, pembe za ndovu, karafuu n.k. Hawa Washirazi walikuwa wakaazi wa Ghuba ya Uajemi na kwa maingiliano yao na wenyeji wa Afrika Mashariki, utamaduni mpya uliibuka.'"

Kuja madarakani 'Toghrul Mseljuki' Shiraz, chanzo cha Mashia kuhama

Murtadha Ridhwanifar mjumbe wa Kituo cha Utafiti cha Shrika la Utamaduni na Utalii la Iran anaongeza kuwa: "Baadhi ya wataalamu wa historia wanasema sababu ya wahajiri Mashia kuhamia katika pwani ya Afrika Mashariki ni kuingia madarakani Toghrul Mseljuki katika silsila ya utawala wa Waseljuki ambao aliingia madarakani mwaka 247 Hijria Qamaria huko Shirazi. Inasemekana mtawala huyo alikuwa akiwapinga Mashia na Ushia.

Uislamu ulipata nguvu Kilwa karne ya 12 Miladia

Murtadha Ridhwanifar aidha anaashiria kupata nguvu Uislamu Kilwa katika pwania ya Tanzania na kusema: "Ibn Batuta, mtalii maarufu Mwislamu kutoka Morocco katika karne ya 12 Miladia alitembelea eneo la Kilwa na kuathiriwa sana kutokana na kuenea Uislamu miongoni mwa wenyeji wa eneo hilo. Aliandika hivi kuhusu eneo hilo, ‘Watu hapa wanaamini kuhusu vita vitakatifu, wanamcha Mwenyezi Mungu na wanatenda amali njema.’”

Sultan Ali kutoka Shiraz: Muasisi wa mji wa Kilwa

Ridhwanifar anaongeza kuwa: " Ibn Masoud mwanahistoria maarufu anasimulia aliyoyaona katika mji wa Kilwa ambao uliasisiwa na Sultan Ali ibn al-Hassan Shirazi na imearifikwa kuwa alikuwa miongoni mwa Mashia kutoka Shiraz na alioa biniye mtawala mwenyeji wa eneo hilo.”

Ridhwanifar anasema Mashia waliofika katika pwani ya Afrika Mashariki walichukua hatua mbili muhimu zenye taathira. Awali ni kuanzisha biashara na hivyo kupelekea eneo hilo kushuhudia ustawi wa uchumi na miji na pia walitoa mchango mkubwa katika kuenea Uislamu eneo hilo ambapo pia walijishughulisha na ujenzi wa misikiti. Ridhwanifar anasema awali Sultan Ali ibn al-Hassan Shirazi alikuwa na makao yake Zanzibar kisha akahamia Kilwa.

Kubuniwa Miji Nchi yenye kijitegemea

Mtafiti Ridhwanifari anasema Washirazi waliendeleza biashara na uchumi na kuunda Miji Nchi (city states) kama ile ya Malindi, Lamu na Anjouan. Miji Nchi hii ilikuwa ikiendeshwa kwa kujitegemea au kupitia mfumo wa majimbo pamoja na kuwa kulikuwa na serikali kuu. Miji hiyo ilikuwa na vyombo vya mahakama na vyombo vya utungaji sheria. Ufalme huo ulianzosha na Sultan Hassan ulisambaratika katika karne za 14-15 Miladia.

Wareno waliwaua kwa umati Wairani

Murtadha Ridhwanifar anasema katika mwisho wa kanre ya 15 Miladia, wakati wa utawala wa Fadhil bin Sulaiman, mwanabaharia maafuru wa Ureno, Vasco Da Gama alifanikiwa kupata njia ya kuenda India kutoka Ulaya kwa kulizunguka bara la Afrika. Baada ya vita na njama, seirkali ya Zainzibar ilianguka. Wareno hapo walianza vita vvya kikatili ambao Wairani na Waarabu waliangamizwa kwa umati.

Mwishoni mwa mahojiano Ridhwanifar anaashiria kuhusu Msikiti wa Kizimkazi , msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki na uko visiwani Zanzibar na ulijengwa na Wairani mwaka 500 Hijria Qamaria sawa na mwaka 1107 Miladia.

Powered by IQNA
 
1. Wahadimu ni watu gani, au asili yao ni wapi?

2. Kwanini Zanzibar ni Sunni Muslims wakati kuna Washirazi ambao ni Shia Muslims?

3. Kwanini hakuna Shia Muslims maeneo ambayo Washirazi walifika ambayo mmeyataja kama Lindi, Mafia, etc.

4. Napenda pia kufahamishwa kuhusu Wayemen walivyokuja Tanganyika. Walifika maeneo gani haswa.

..Naomba mnivumilie kama kuna mahali nimekosea. I am ignorant about this subject.

Cc Mohamed Said
 
1. Wahadimu ni watu gani, au asili yao ni wapi?

2. Kwanini Zanzibar ni Sunni Muslims wakati kuna Washirazi ambao ni Shia Muslims?

3. Kwanini hakuna Shia Muslims maeneo ambayo Washirazi walifika ambayo mmeyataja kama Lindi, Mafia, etc.

4. Napenda pia kufahamishwa kuhusu Wayemen walivyokuja Tanganyika. Walifika maeneo gani haswa.

..Naomba mnivumilie kama kuna mahali nimekosea. I am ignorant about this subject.

Cc Mohamed Said
Wazanzibar wengi ni ahmadiyah sunni wachache
 
Wazanzibar wengi ni ahmadiyah sunni wachache

..kwa mtu asiye na ufahamu na imani ya Kiislamu naweza vipi kumtofautisha Sunni na Ahmadiyah?

..kwa mfano, Dr.Hussein Mwinyi ni Ahmadiah au Sunni? Na Sheikh Abeid Karume alikuwa Sunni au Ahmadiyah?
 
Ok.nimepitia kwanza sayyed na ali sio watu wawil isipokuwa ni mtu mmoja.sayydna Ali (r.a) .huenda maelezo yako yakawa na kweli kwamba fitna kuubwa iliibuka kwa asil ya shia kwamba aliyetakiwa kuchukua ukhalfia baada ya kifo cha mtume wanasema alipaswa kuwa Ali na sio abubakar.
Kilichofanya jamii za arabun kuselelea mwing pwan ya africa masharik ni ule uwezo waliokuwa nao na technology ya kutengeneza vyombo kwa maana ya jahaz zenye uwezo wa kuingia maji makubwa na elimu ya nyota kuwenda kutumia kama dira(compass) .
Hassan bin ali alifika kilwa akitokea uajem na kukinunua kisiw kwa jora la kitambaa kuzunguka kisiwa.sijafahamu walipima vip ila alimpa mtawala wa pale jora la kitambaa.bado waliweza kueenea kote mpaka tongoni huko tena ndio kunafahamika kabisa ni magofu ya washiraz
 
Back
Top Bottom