Je atapita tu kwa muda, yupo atakayechukua ipasavyo?

Je atapita tu kwa muda, yupo atakayechukua ipasavyo?

Joined
Nov 5, 2021
Posts
40
Reaction score
24
Habari wana Jamii wenzangu.....

Nimejitokeza kwa mara ya kwanza katika jumuia hii nikiwa na mtazamo binafsi kwa haya yanayotokea katika serikali yetu haswa Chanzo chake kikiwa ni Deni la Taifa lililosababishwa na awamu zetu zote za utawala kwa kuzingatia màhitaji ya wakati huo na sasa Kupitia sera nà ilàni na mipango ya maendeleo inayotekelezwa kwa awamu kimkakati....

Nachojiuliza na kuwaza hii mikopo tunayokopa kama Nchi ukiondoa kuwa inatumika kutekeleza baadhi ya Miradi yetu je nyuma yake kuna watu ni wanufaika kwa baadhi ya mikopo ikiwa nà agenda ya Siri kinyume na Taifa harafu mlipaji ni Mtanzania mnyonge na Masikini,machinga,Boda boda na Mama ntilie...Nasema haya kutokana na mambo yanayoendelea ambayo kwa ustawi wa Taifa letu hayapendezi hata kidogo.....

Kwani ninapoona mihimili ya Nchi yetu tukufu ikikinzana kimtizamo hadharani maana yake vikao vya ndani vimeshindwa kuleta Muafakà wa kitaifa na kuleta makundi matatu ndani ya utawala ambayoni .....1) Kundi la wanaokubaliana na yanayoendelea.2)kundi la wasiokubali yanayoendelea na 3) Kundi la wasiokuwa na upande wowote ambalo ni Kundi baya sana...hili Kundi la tatu liko kimya halisemi kitu ila linamalengo mabaya juu yetu watanzania....

Hili Kundi liko nyuma ya maamuzi sahihi na yasiyo sahihi namaanisha liko nyuma ya kundi la kwanza na la pili na lengo lake ni kuhujumu ustawi wa kisiasa wa Taifa letu hili ndilo kundi lenye lengo KUU la kukidondosha Chama Cha Mapinduzi madarakani .......linatumia Agenda ya katiba mpya na Agenda ya Deni la Taifa likihusisha Miradi mikubwa Mikubwa inayoendelea sasa.....likiwa na dhamira ya kuwashitaki viongozi wetu waliopo madarakani kwa wananchi likitumia hizo Agenda likitoa ushauri mbaya na kwa kiasi kidogo mzuri...

Baada ya Agenda ya katiba mpya kushindwa kuleta matokeo Chaya kwa kundi hili la tatu sasa limefanikiwa kuyagombanisha makundi mawili kwa Agenda ya Deni la Taifa hivyo wasiwasi wangu ni namna kundi hili litakapo chukua Nchi Kupitia CCM kisha litamaliza Muda wa miaka 10 ya Uongozi limekipasua Chama kàtikati na kupoteza sifa kwa Watanzania kwa jinsi litakavyokuwa limeiharibu Nchi vibaya kwa kugawa rasilimali zetu kwa mabeberu kama utii baada ya kuingia madarakani Kupitia mabeberu hao wa magharibi.....

Hivyo kwa haya yanayoendelea Mama Bado anao mda wakae kwa pamoja na familia zote tatu yaani yeye na mihimili Mingine miwili....(Bunge na Mahakama) kama viongozi wavivae viatu vya Baba kwa kuweka sawa tofauti zote zilizojitokeza,Kisha walikatae Hilo kundi la tatu lisilo na nia njema na Mama na hao wote waliokuwa na Baba kwani kwa pamoja katika sekta ya uchumi na Maendeleo walitufariji sisi watanzania wanyonge na tuliwapenda sana....

Isije kuwa Mama anapita tu kwa muda, yupo wa upande wa kundi la tatu ataichukua Nchi ipasaavyo kisha atuzamishe Kwa masirahi ya kundi lake na Mabeberu wasio na huruma nasi toka enzi za utumwa,waliwatesa Babu zetu wanaturudia na sisi kwa kuwatumia walio miongoni mwetu waliokuwa wamedhamiria kuing'oa na kupoteza CCM 2015 Hali ya kuwa wao pia CCM imewajengea Heshima kubwa ila kwa fedha za kigeni Wanaisariti CCM na watanzania wanyonge.... Ahsanteni
 
Sema deni limesababishwa na awamu ya tano, kuwakataa mabeberu ni sawa na kuyakataa maji , ambayo yanaumuhimu kwa kila secta.
 
Sema deni limesababishwa na awamu ya tano, kuwakataa mabeberu ni sawa na kuyakataa maji , ambayo yanaumuhimu kwa kila secta.
Kwa ninavyofahamu mm kumuhitaji mtu hilo sio kosa lakini kosa mtu huyo baada ya kuona unamhitaji anakutumia kwa masirahi yake na Taifa lake hilo ni kosa kubwa sana Boss.....Tunawahitaji mabeberu sikatai lakini namna tunavyokwenda kwao na kujieleza tunatengeneza mianya ya kuingilia mpaka mifumo yetu ya kiutawala...kosa ni letu wenyewe..
 
Back
Top Bottom