Ahsante kwa ufafanuzi, hoja yangu inalenga kufahamu ikiwa imevunjwa na kadhi
Asante sana,
Kama umekubali kurekebisha kauli sasa ngoja tuendelee na swali lako.
Kwanza swali lako lipo kwa jumla sana hivyo tutalijibu kwa jumla hivyo hivyo
Tanbihi muhimu kabla sijaendelea niiweke kwenye neno KUMREJEA. Kumrejea mke kwenye uislamu inajulikana kama kumrudia mke ambaye umemwacha kwa talaka moja au mbili. Kwahiyo kama neno hilo umelitumia kwa maana hiyo jibu lako litakuwa ni HAPANA, NDOA IKIVUNJWA MAANA YAKE HAIPO TENA HIVYO HUWEZI KUMREJEA. Kama sababu za kuvunjwa zikiondoka kisha vigezo na masharti vikatimia utaruhusiwa kumrudia mke huyo kwa kuanza upya kabisa yaani atakuwa mkeo kwa NDOA MPYA
Twende sasa kwenye ufafanuzi
Kisheria ndoa huweza kuvunjwa na kadhi kwa sababu mbalimbali. Kutokana na sababu hizo ndipo tunaweza kujua kwamba mume anaruhusiwa kumwoa tena huyo mwanamke au laa
Mfano ndoa ilivunjwa kwa sababu ya mume kuwa na mateso ya kusudi, kumtelekeza mke, kutomtimizia haki za kindoa nk kisha baadae akajirekebisha basi hapo akimtaka mkewe ataruhusiwa kumwoa kwa kuanza upya kabisa (wanapatana mahari na taratibu zingine zote za ndoa zinafuatwa kama kawaida). Sababu nyingine ambazo zinasababisha ndoa kuvunjwa na zinaweza kuondoka sababu hizo mkaruhusiwa kuoana ni mfano ndoa kuwa ni ya tano kwa mwanaume na nne zilizotangulia zote ziko hai, mke kuwa kwenye ndoa nyingine, nk
Lakini unakuta tuchukulie mfano mmoja tu, ndoa ilivunjwa kwa sababu imebainika mume na mke ni maharimu hapo hata ufanyaje huwezi kuruhusiwa kumuoa huyo mwanamke, daima!
Narudia tena kwa kukazia jibu,
Mume peke yake ndiye mwenye mamlaka ya kutoa talaka na kwenye talaka ndipo kuna habari ya kurejea mke akawa mkeo tena bila ya kufunga ndoa upya. Kinyume na hapo, ndoa ikivunjwa na kadhi maana yake imebatilishwa yaani haipo hivyo mwanaume akimtaka huyo mwanamke wataanza kila kitu upya kabisa kama hawakuwahi kuoana vile
Vilevile nakazia jibu kwamba kuna sababu za kuvunjwa ndoa zinaweza kuondoka na mkaruhisiwa kuoana tena lakini kuna sababu nyingine haziwezi kutoweka kamwe na itabaki kuwa ni haramu nyinyi kuoana
Wallaahu a'alam