BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Wakenya wamechachamaa sana na Mswaada wa bajeti yao, wanaona hauna maslahi kwao, Pamoja na kufanyiwa mabadiliko bado wanachachamaa tu.
Wakenya wako chonjo na Bajeti yao wanapitia kifungu kwa kifungu. Mijadala yao mikuu kwa sasa ni bajeti yao tu hakuna mjadala mwingine.
Njoo Tanzania kwenye vyombo vya habari hasa Redio na Television ni mada za Yanga na Simba kutwa nzima, au mada za Mahouse Girl, Mama na Baba wa Kambo, mada za kufumaniana, maada za kusutana, baadae Taarabu na siku inakuwa imeisha.
Vijiwe vya kahawa na Tangawizi mada kuu ni Yanga na Simba, habari za Bajeti hazituhusu kabisa au labda mtu kama Mbowe au Lissu waandamane kwa niaba yetu, then sisi ikifika saa 2 usiku tukae pembeni ya Tv tukiangalia jinsi wanavyopigwa mabomu ya machozi baada ya hapo sasa tutaingia kwenye makundi ya WhatsApp, X, Facebook na humu kuja kulalalmika.
Hakuna Taifa lina raia wasiojali kama hii Tanzania kama lipo Taifadhali tuambizane hapa, na hii ni neema kuu kwa watawala, wanagawana nchi wakijua fika raia wale sana wanajua kubisahana kuhusu Yanga na Simba.
Bajeti itapitishwa bila aina yoyote ile ya upinzani hata wa danganya toto, na hakuna unafuu utakaopatikana na mwakani tena watakuja na Bajeti nyingine na tutaambiwa hii ni bajeti ya wananchi.
Tunataka either Mbowe au Lissu au mtu mwingine yoyote au hata Maaskofu wa TEC au Shura ya Maimamu walalamike, wao ikibidi waandamane kwa niaba yetu sisi, au watusemee kabisa.
Mpina anapambana mwenyewe kana kwamba familia yake ndio pekeee iko affected na sakata la Sukari, sisi haituhusu kabisa.
Huu ukimya na ukondoo ni Neeema kuu kabisa kwa watawala.