Je, Bajeti yetu ni Bora sana? Mbona tuko kimya sana? Vijana Kenya wanaandamana

Je, Bajeti yetu ni Bora sana? Mbona tuko kimya sana? Vijana Kenya wanaandamana

Wakenya wamechachamaa sana na Mswaada wa bajeti yao, wanaona hauna maslahi kwao, Pamoja na kufanyiwa mabadiliko bado wanachachamaa tu.

Wakenya wako chonjo na Bajeti yao wanapitia kifungu kwa kifungu. Mijadala yao mikuu kwa sasa ni bajeti yao tu hakuna mjadala mwingine.

Njoo Tanzania kwenye vyombo vya habari hasa Redio na Television ni mada za Yanga na Simba kutwa nzima, au mada za Mahouse Girl, Mama na Baba wa Kambo, mada za kufumaniana, maada za kusutana, baadae Taarabu na siku inakuwa imeisha.

Vijiwe vya kahawa na Tangawizi mada kuu ni Yanga na Simba, habari za Bajeti hazituhusu kabisa au labda mtu kama Mbowe au Lissu waandamane kwa niaba yetu, then sisi ikifika saa 2 usiku tukae pembeni ya Tv tukiangalia jinsi wanavyopigwa mabomu ya machozi baada ya hapo sasa tutaingia kwenye makundi ya WhatsApp, X, Facebook na humu kuja kulalalmika.

Hakuna Taifa lina raia wasiojali kama hii Tanzania kama lipo Taifadhali tuambizane hapa, na hii ni neema kuu kwa watawala, wanagawana nchi wakijua fika raia wale sana wanajua kubisahana kuhusu Yanga na Simba.

Bajeti itapitishwa bila aina yoyote ile ya upinzani hata wa danganya toto, na hakuna unafuu utakaopatikana na mwakani tena watakuja na Bajeti nyingine na tutaambiwa hii ni bajeti ya wananchi.

Tunataka either Mbowe au Lissu au mtu mwingine yoyote au hata Maaskofu wa TEC au Shura ya Maimamu walalamike, wao ikibidi waandamane kwa niaba yetu sisi, au watusemee kabisa.

Mpina anapambana mwenyewe kana kwamba familia yake ndio pekeee iko affected na sakata la Sukari, sisi haituhusu kabisa.

Huu ukimya na ukondoo ni Neeema kuu kabisa kwa watawala.
Maandamano ambayo wabongo wanayaweza ni ya simba na yanga, bongofleva, zaidi ya hapo hawana guts
 
Nenda Kenya Sasa badala yakuweka hoja unaleta mapenzi na nchi za watu Tanzania ni Tanzania Kenya ni Kenya ,hatuishi kuangalia wao wanafanya Nini na sisi tuwaige hii ni nchi mapokeo yetu ni tofauti na wao vile vile huku bajeti imeanza kuchambuliwa tuu vizuri
Huku bajeti inaweza kuwa nzuri ila upigaji unakuwa mwingi we sikilizia ripoti ya cag
 
Huku bajeti inaweza kuwa nzuri ila upigaji unakuwa mwingi we sikilizia ripoti ya cag
Ni kweli mkuu ila napingana na mleta mada kwamba Kenya wamechachamaa na sisi tuchachamae,
 
Weka ayo mapungufu tunajadili kwa ufupi Bado bajeti haijapitishwa
kuweka ushuru kwenye magari ya umeme na gas ni UJUHA wa hali ya juu, yaani badala ya kuondoa KODI ili watu watumie gas na umeme zaidi kuliko mafuta wao wanaongeza USHURU na Kodi.

Pili, bajeti haizungumzi wala kutaja chanzo kipya (yaani ubunifu) wa namna ya kukusanya kodi, kila siku ujinga ni ule ule, hizo levy, taxes ziko kama zote. Mazingira kama haya huwezi kusema kuwa tuna bajeti nzuri, tuna ujinga kiwango kikubwa
 
Kwa sasa Tanzania tuna tatizo moja kubwa nalo ni CCM
Kila tatizo tulilonala la rushwa, ufisadi, bajeti mbovu, waandishi wa habari wa kicomedy kama alivyosema Tido Mhando,
Na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo ni kwa sababu ya ccm
Wewe fikiria kiongozi wa nchi anajifananisha na chura huku wapambe waje wakimfananisha na mitume

Waziri wa fedha anawaza yanga
badala ya kuja na suluhisho na jinsi ya kuimarisha shilingi yetu isiendelee kuporomoka thamani.
 
Nimekuwa Mfuasi wa siasa za Kenya kwa muda sasa, imefikia sehemu nahisi labda wao wametokea Sayari tofauti na hii tunayoishi WABONGO. Juzi vijana wamemwagika barabarani kupinga Muswada wa fedha uliokuwa imejaa kodi kibao na hatimae "ZAKAYO AKASHUKA" Huku Bongo tuliambiwa kama hutaki kulipa uhamie Burundi😥😢😢. Swali la msingi, Wakenya wanatokea Sayari gani? Hapa kwetu kwanini haiwezekani?
 
duh! labda tumeridhika na nchi yetu!
 
Je,
1. Tumekubali kuwa Moshi unaozunguka Kutwa umeshatuathiri hadi Ubongo?
2. Tumerogwa tokea Taifa linaundwa?
3. Hatujitambui?
4. Kiuhalisia hatuna Akili?
5. Elimu yetu ni tatizo?
6. Roho ya Ujasiri na Uthubutu ilipita kwa bahati juu ya Mbingu yetu na kwenda Kwingineko?
7. Tuna Laana ya Kutukuka ya Unafiki na Uwoga?

Ninayasubiria majibu yenu ila nadhani sasa ni high time nizae na Mwanamke wa Kenya ili nimpate Mtanzania Jasiri.
 
Je,
1. Tumekubali kuwa Moshi unaozunguka Kutwa umeshatuathiri hadi Ubongo?
2. Tumerogwa tokea Taifa linaundwa?
3. Hatujitambui?
4. Kiuhalisia hatuna Akili?
5. Elimu yetu ni tatizo?
6. Roho ya Ujasiri na Uthubutu ilipita kwa bahati juu ya Mbingu yetu na kwenda Kwingineko?
7. Tuna Laana ya Kutukuka ya Unafiki na Uwoga?

Ninayasubiria majibu yenu ila nadhani sasa ni high time nizae na Mwanamke wa Kenya ili nimpate Mtanzania Jasiri.
Changamoto za Kundustan sio sawa na Changamoto za Tanzanian.

Pili Wanasiasa wa Upinzani ni matapeli Wameshindwa Kila Nchi walikoshika Dola kuanzia Ghana Hadi Malawi to Kenya.Walichoahidi sicho wanafanya.

Hapa Tanzania mama ni msikivu na Huwa anafanya Yale ambayo Watanzania wanapenda.Sasa umjambishe Kwa lipi labda?
 
Back
Top Bottom