Je, Bajeti yetu ni Bora sana? Mbona tuko kimya sana? Vijana Kenya wanaandamana

Je, Bajeti yetu ni Bora sana? Mbona tuko kimya sana? Vijana Kenya wanaandamana

WADANGANYIKA aliyeturoga kafa, sisi ni watu wa hewala hewala sana, wachache tumekuwa keyboard warriors, wengine machawa, wengine walilishwa sumu ya amani muhimu.
 
Sehemu kubwa ya Watanzania ni kama watu waliokufa, hawajui haki zao, hawajui kinachoendelea wao ili mradi mtu anapata ugali wake na analala basi kwake imetosha.

Watu wamejaribu kuwaamsha lakini wapi, ni kama kumuamsha marehemu, hata umpige shoti ya umeme haamki.

Ndio maana watu wenye akili wameamua tu watulie, na wao wakipata kula basi wale watulie maana ni vigumu kufundusha mtu haki zake na bado hataki kuelewa.
 
Wabongo tuna tatizo mahala, huu ukondoo tulionao ni zaidi ya kawaida ndio maana inasemekana Kenyatta baba wa taifa la Kenya aliwahi kumwambia Nyerere anaongoza maiti, serious sisi ni maiti zinazotembea.

• Bandari imetolewa bure kwa waarabu - Kimya.

• Uwanja wa KIA umetolewa kwa waarabu - Kimya.

• Sehemu ya bahari imetolewa juzi kwa Wakorea - Kimya.

• Bashe anatupiga kila siku anavyotaka - Kimya.

• Ngorongoro/ Loliondo zimetolewa kwa Waarabu - Kimya.

• Sehemu ya misitu yetu inakadiriwa kufikia hekta 8000 imetolewa kwa Waarabu - Kimya.

• Betina kule bungeni anamtisha Mpina -Kimya.

What else on earth will make us react?!
 
Back
Top Bottom