Je, biashara ya Movie Library na Play Station (PS) bado zina soko kwa sasa?

Je, biashara ya Movie Library na Play Station (PS) bado zina soko kwa sasa?

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Habari zenu wakuu.

Mapambano yanazidi kupamba moto kila uchwao, kila mmoja katika nafasi yake. Leo nimekuja na swali kwenu nyote wataalamu katika masuala ya kusoma upepo wa biashara kule ziendako kutoka na mabadiliko ya kidunia. Kama tujuavyo kwa sasa duniani iko kasi sana kwenye suala zima la teknolojia.

Kuna hizi biashara mbili, Movie Library na Play Station (PS) hizi biashara kwa miaka ya nyuma watu wametengeneza pesa sana, japo watu walizichukulia poa ila kuna baadhi waliingiza pesa sana. Mpaka sasa bado kuna watu wanazifanya huko mitaani kila mmoja kwa namna yake.

Dunia iko kasi sana kwa sasa na mambo mengi hubadilika kutokana na nyakati. Swali langu ni kuwa hizi biashara mbili kwa nyakati hizi na miaka 5 mbele je, bado zina soko? Tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya ki teknolojia, je hizo biashara bado hazija asiliwa na kukuwa kwa teknolojia vipi kuhusu miaka mitano mbele?

Wale wataalamu wa kusoma upepo wa biashara kutokana na nyakati naomba mtufahishe jambo hili, hii itasaidia kabla ya mtu kuingia huko ajue cha kufanya.

Karibuni nyote kwa maoni.
 
Mie kuna sku nkasema ngoja nkaweka movie kwa mwanangu ile naweka ya kwanza nkajikuta nmeweka movie 5 na season 2 kumbuka movie 1 ni buku season 2k.

Na hapo kuna wengine walikuwa wanakuja kuweka mpka 500gb so ni biashara inayolipa mno sema bongo kila biashara inayolipwa watu wanafanya kama siri kimyaa
 
Movie utadownload ofisini km kuna WiFi.
Hila hiyo biashara mimi siiwezi, wanaodownlodigi wapo nawaacha wakimaliza nampa tu external aniwekee.

Au unaenda movie store buku 2 tu
Kwenye biashara kitu Cha kwanza ni kutarget soko lako, jiulize wangapi wa access ya kupata wifi Tanzania hii??

Movie store unaweza kumpa dogo buku 5 ukaenda na external ukaweka hata movie 50 Wala hawanaga noma, sasa jiulize useme u download mwenyewe? Gharama na muda???
 
Kuna kitu unaweza kuongea ukaonekana limbukeni bila kujijua, unajua gharama za kupakua movie Moja tu let's say Ina 1.3 gb?
Huyo jamaa ni limbukeni tu, anajiona wa kishua sana. Kama hadi Sasa uswahilini bado Kuna watu kibao wanatumia deki za DVD hiyo biashara itaendelea kulipa hata miaka 15 ijayo, sababu sisi tupo nyuma kiteknolojia kama miaka 30 au zaidi. Chukulia bado Kuna watu kibao wanatumia Simu za tochi tena zisizo na memory card, wakija kununua smart phone si ndo watakuwa wateja wako wa kuweka miziki kwenye simu!?,kumbuka biashara ya movie haiendi peke yake. Lazima uwe na PC ya kuweka miziki kwenye simu pia.
 
Biashara za uswahilini hizo mkuu.
Au labda kama unataka iwe classic movie na Ps basi fungua karibu na maeneo wanakoishi wanachuo(huku sio za kutafsiriwa)

Au maeneo ya kishua(huku pia sio za kutafsiriwa) ofisi za maeneo haya huwa classic safi za unyama flani hivi wa tofauti.

Hizi za uswahilini naonga hata hazina mtaji mkubwa, viti vya lazima ni spika nje, komputa yako, makasha ya cd kadhaa ya kuanzia, seasons zinazopendwa na kufuatilia mwendelezo wake.
Wateja wengi wa uswahilini ni watoto wa shule, kipindi cha likizo naonaga wanajaa muda wote ila shule zikifunguliwa naskiaga wazazi wanakua wakali kwa wamiliki wa hizo ofisi, ila weekend pia ni siku ya maokoto.
 
Mm mkuu nakaa masaki lakin naenda kuweka muvi kwa dj mack kariakoo
 
Back
Top Bottom