Je, biashara ya Movie Library na Play Station (PS) bado zina soko kwa sasa?

Je, biashara ya Movie Library na Play Station (PS) bado zina soko kwa sasa?

Kwa maoni yako bado inalipa
Biashara za uswahilini hizo mkuu.
Au labda kama unataka iwe classic movie na Ps basi fungua karibu na maeneo wanakoishi wanachuo(huku sio za kutafsiriwa)

Au maeneo ya kishua(huku pia sio za kutafsiriwa) ofisi za maeneo haya huwa classic safi za unyama flani hivi wa tofauti.

Hizi za uswahilini naonga hata hazina mtaji mkubwa, viti vya lazima ni spika nje, komputa yako, makasha ya cd kadhaa ya kuanzia, seasons zinazopendwa na kufuatilia mwendelezo wake.
Wateja wengi wa uswahilini ni watoto wa shule, kipindi cha likizo naonaga wanajaa muda wote ila shule zikifunguliwa naskiaga wazazi wanakua wakali kwa wamiliki wa hizo ofisi, ila weekend pia ni siku ya maokoto.
 
Kwenye biashara kitu Cha kwanza ni kutarget soko lako, jiulize wangapi wa access ya kupata wifi Tanzania hii??

Movie store unaweza kumpa dogo buku 5 ukaenda na external ukaweka hata movie 50 Wala hawanaga noma, sasa jiulize useme u download mwenyewe? Gharama na muda???

Kweli Kabisa Tanzania, Wifi Ni kwa wachache sana
 
Kudownload kitu online inahitaji uwe na ujunzi maana site zipo nyingi sana na sio kila site zina movies hd,unaweza kudownload movies ikawa low quality au ikashindwa kuplaya kwenye TV,lila TV zinazotoka sasa lazima ujue code zake lasivyo utakuwa unawaza maji kwenye gunia,alafu kudownload movies inahitaji uwe na wifi maana kuitumia mb za hii mitandao itakata faster utanikuta download movies ya GB 1 kwa kutumia GB 5 maana internetbitakuwa inalika kwa ads za site au simu itakuwa inaji update yenyewe au app za simu,ili use na movies shop lazima uwe na internet ya kueleweka kama mimi nalioia kwa mwenzi 11000 unlimited
Kiongozi muongozo kidogo kuhusu unlimited hio🙌
 
Pia PM yako kiongozi tuyajenge zaidi
 
Ok nimewafuatilia comments za kila mmoja huku kunawanaojua vyema hii biashara na wengine hawajui kitu,hii business nimeifanya toka 2018 kipindi hicho naanza nilikuwa na computer ya quare 2 duo na external ya 1tb jumla nilikuwa na storage GB 1500 na nikianza kwenye kibanda cha mtu yeye pia alikuwa anaifanya hii biashara sasa computer zake ziliharibika akawa hana jinsi akaona anikodishie.
Basi nikaanza kwa kusua sua na CD kama 15 za rango,chandraagupta,Aladdin, na udaani basi nikakomaa nakumbuka kwa siku nilikuwa naaingiza 1500 tena hapo naweka tu nyimbo basi,Sikh nzima na shinda officine nasikiliza nyimbo tu,siku kata tamaa nimekomaa mpaka sasa nina computer 2 za maana moja inamovies za kutafsiriwa tu nyingine zisizotafsiriwa kwa storage niliyokuwa nayo sasa tb 20 za movies za kutafisiriwa na TB 24 za movies zisizotafisiriwa aisee naaingiza pesa kinyama siju biashara ikiwa vinzuri naaingiza mpaka elfu 50 siku ikiwa mbaya elfu 25 mpaka 30 uniambii kitu kuhusu hii biashara naijua A to Z kwangu ukija ukosi kitu kama sina naidownload maana nina router ya airtel nailipia kwa mwenzi aisee nimejipanga
Mkuu naomba nikuulize maadam una uzoefu. Hivi hii biashara ukimuweka mtu kibandani akufanyie kazi na wewe kama boss, unaweza kuisimamia vipi, hesabu yake mnapigaje na mnalipanaje...?
 
Back
Top Bottom