johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,639
Uwepo wa upinzani katika mfumo wa kisiasa kuna faida na hasara zake.
Moja ya faida ni ile ya kuusingizia upinzani kila wakati mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo.
Hata kwenye dini pasingekuwepo shetani basi sifa na shutuma zote zingekuwa zinapelekwa kwa Mungu lakini sasa uovu huelekezwa kwa shetani japo anayeutenda ni binadamu.
Wakati CCM ikijikita kwenye kuufuta upinzani kwenye ramani ya siasa ikumbuke pia wapinzani wakiisha shutuma na madongo ya wanasiasa yataanza kuelekezwa kwa viongozi wake.
Tusisahau kuwa wanasiasa wa " kweli " hutafuta kusifiwa na wananchi siyo viongozi tulioishi wakati wa Nyerere tunalikumbuka hilo.
Hivyo viongozi wa CCM na hasa wale wenye makandokando wajiandae, hawa akina " Lijualikali " Mbowe na Chadema wakiondoka watatafuta wa kuwatupia madongo ndani ya CCM ili waendelee kusikika.
Nawatakia Eid pili yenye baraka.
Maendeleo hayana vyama!
cc: Wakudadavuwa