Je, bila ya Diamond, muziki wetu utasonga zaidi ya hapa?

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Tuweni wakweli wadau,

Hivi siku ukisikia Diamond Platinumz kaacha mziki au kafa (siombei itokee) utajiskiaje? Na vipi kuhusu muziki wetu wa Tanzania kwa ujumla unahisi kuna mtu anaweza akausogeza zaidi ya hapa ulipo?

Kwa maana leo nimekaa naskiliza nyimbo zake tangu enzi hizo za Kamwambie mpaka hii ya sasa hivi ya Salome nikaona daah huyu jamaa akiacha mziki kama Suma Lee itakuwa ndio basi tena kwa mziki wetu kupiga hatua.

Kama vile wapenzi wa Bongo Movie walivyoondokewa na Kanumba au wapenzi wa Taarabu walivyoondokewa na Yusuph, mwisho wa siku ndio kama hao akina Thabit wanataka mziki wao upigwe kanisani.





 
Hili swali ukimuuliza Ray kigosi au mtu yeyote wa bongo muvi atakujibu sawia kabisa mkuu
 
Kwani yeye ndo nani?
Kabla ya D hapakuwa na mziki?
 
Anachokifanya Alikiba sahivi ni kama alichokuwa akifanya Ray wa wakati wa Kanumba, alionekana anajua kwavile alikuwa anasafiria nyota ya jamaa, alipoondoka kanumba ndio tumemjua Ray halisi ni nani, maana kashindwa kusogea kabisa, ingekuwa Kanumba anarudi angeshangaa kuona Ray amebakia palepale alipomuacha, kilichoongezeka ni kunywa maji sana na mahaba na chuchu hans
 
Hatakama anamapungufu lakini Diamond Lazima apewe heshima yake,
 
Team Diamond
Team Kiba
Zitapotea na kupungua nguvu hivyo ushindani wa kimziki wa Ali kiba utapungua nguvu katika soko la mziki wa bongofleva.

WCB itabaki jina japo mameneja watajitahidi kadri wawezavyo.

Madensa, cameraman na ambao wapo nyuma ya diamond watapoteza muelekeo na hata kuondoka WCB.

Kidogo kidogo channel za kupiga show kimataifa zitapungua na mziki wa bongofleva utapungua soko lake na mwishoni wengi wataacha mziki halafu wafanye biashara nyingine.

Babu tale atachoka na kurudi nyuma hata kimaslahi kwenye mziki anaweza kujikita kwenye shughuli za biashara, Sallam Sk atakuwa meneja wa kujitegemea. Mali za Diamond zitapotea potea na kuuzwa

Gharama za show stejini zitapungua kidogo kidogo kwa wasanii. Mama Diamond na esma watakuwa wakawaida ila Tiffah atakuja kuwa supastaa baadae kupitia malezi ya zari.
 
Waulize bongo movie, hadi leo hawajaweza kuziba pengo la Kanumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…