Abuu Said
JF-Expert Member
- Jul 5, 2015
- 4,010
- 4,763
Habarini wana Intelligence ....
...hili jambo linanichanganya sana juu ya uwepo wetu Duniani....
Nikiangalia vitabu vya Dini zote vinatuambia kwamba, lengo la kuumbwa kwetu Mungu alitaka kiumbe kitakachoweza kuitawala Dunia na vilivyomo ndani yake.
Sasa hapohapo vitabu vya Dini vinatuambia Binaadamu wa kwanza kuumbwa aliwekwa Heden kwa tafsiri rahisi ni sehemu iliyokuwa tulivu yenye Miti, matunda na Bustani za kupendeza zilizopo hukohuko Mbinguni then Adam akaumbiwa mwanamke ili amfariji na wazaane....
.....vitabu vya Dini vikaendelea kutupa historia yetu sisi wanaadamu kwamba baba yetu Adam na Mama yetu Hawa walikosea masharti waliyowekewa kuishi humo kwa kurubuniwa na Malaika mmoja mkosefu aliyekataa kumsujudia Adam basi Adam na Hawa wakatupwa Duniani.
.....sasa maswali yapo hapa...
Kama lengo la Mungu kumuumba mwanaadam kuja kuitawala Dunia kwanini alimweka kwanza Mbinguni na asinge mleta moja kwa moja Duniani mpaka pale alipokosea?...
Inaelezwa kwamba Malaika Ibilisi ndie alie warubuni Adam na Hawa Je ulikuwa ni mpango wa Mungu awajaribu na kupata sababu ya kutuleta Duniani?
Je kwanini Mungu aliona hii ndio njia bora na si kututeremsha kwa Amani na akatuchagulia njia ya kumkosea?
Je kuna mapungufu katika hili juu ya uwepo wa binaadam Duniani. Nawaombeni wana Jamvi tujadilini hili
NAWASILISHA
'HOW MUCH IS TOO MUCH?'