Je, Binadamu tuna free will (Hiari)?

Mkuu tunaongea kuhusu ‘free will’ hatujafika kwenye uhalali au uharamu wa dhambi. Tutafurahi sana ukitupa mchango wako kwenye mada husika.
 
kuna mwingine yupo hapo ila njia pekee anayoiona ni A, yani kutokana na sababu zilizo nje ya uweo wake haoni njia X,H,D nk..yeye anaona njia moja tu A...Je huyo tutasema ana free will??
‘Free will’ anayo, ni juu yake kuyakabili hayo mazingira yanayomfanya asione X,H,D, ila amechagua kusema mazingira yamembana na anapaswa kuyakabili ili yamruhusu.
 
Free will ipo mkuu ila watu wengi huwa hawaelewi kwamba uhuru una mipaka. Yan hakunag uhuru usio na mipaka kwasbb kila kiumbe kipo chini ya sheria(Law) na effect hutokea pale ambapo mtu anatak kuwa zaid ya sheria ambay ndio mipaka.

Mfano; Watu huwa wana judge kwamba kam Mungu katupa uhuru kwann anatuadhibu tunapotenda mabaya, lakn wanasahahu huo uhuru waliopewa na Mungu ulikuwa na condtion kwamb ukifanya kitu fulan matokeo yake yatakuwa 1,2,3
Concept yangu ni kwamba kila uhuru una condition kwasbb no one is above the law.
 
St. Augustine, mwanafalsa wa kale aling'ang'ania sana kuhusu free Will, ila Mimi napinga kwa nguvu zote. Hata kama umeuwa kwa makusudi, sio wewe ila Kuna shetani amekusukuma. Swala la Mbinguni na motoni, hakuna mtu anaechagua kwenda motoni ila tangu mwanzo ulishaumbwa ni wa motoni (pre-destination).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…