5. Brain Wiring: Neuroscientists wamegundua kuwa ubongo unafanya kazi kama kifaa cha umeme kupitia miunganiko maalumu ya neurones. Hizi seli ndani ya ubongo (Neurones) zimeungana na kutengeneza pathways (circuits) tofauti tofauti. Kuna neurones zaidi ya billioni 100 kwenye ubongo na kila neurone inaweza kuungana na neurones zingine jirani mpaka 1000. Kwahyo possible combinations ni ngapi hapo wanamahesabu?
Hiyo ni nje ya point, lakini point ni kuwa hizi circuits ndogondogo kwenye ubongo ndio hufanya specific functions,
iwe ni circuit kwa ajili ya kucontrol mapigo ya moyo au circuit kwa ajili ya kunyanyua kidole gumba au circuit kwa ajili ya kusema I love you (Nasimplify lakini its a lil bit complex than that na bado hatujui vingi kuhusu hili).
Ndiomaana huwa ngumu kubadili tabia ya mtu kwa siku moja (Mfano introvert kuwa extrovert,mvivu kuwa mchapakazi au Katili kuwa mpole nk.) kwasababu tayari circuits zinazotengeneza hizo tabia zinakuwa tayari zimeshajitengeneza,ili ubadili inabidi uache kutumia hizi circuits na uanze kutumia zingine zenye tabia mbadala. ambayo huwa ngumu and near impossible kuzifuta circuit zilizokwisha kujitengeneza.
Sasa kama tabia zetu,matendo yetu,mawazo yetu ni miunganiko ya circuits ndani ya ubongo ambazo huwezi kuzicontrol, utasemaje una free will?
Kuna vifaa vinavyoweza kupima activity ya ubongo na imeshagundulika experimentally kuwa kabla conscious mind yako haijafanya maamuzi yoyote mf. kunyanyua kidole, subconcsious mind inakuwa tayari imeshaamua..Kuna vifaa vinaweza kupima hizi neuurones za subconscious na wanasayansi wanaweza kuvitumia kutabiri utafanya nini milliseconds kabla wewe mwenyewe hujaamua utafanya nini. Na wanakuwa sahihi 99% of the time.
6. Determinism: Hii ni imani kuwa ulimwengu unatabirika, yani hali ya ulimwengu ulivyo sekunde hii ndio itakayoathiri na kuleteleza hali ya utakavyokuwa baadae. Maana yake ukijua hali ya kila kitu kilivyo sasa basi unaweza kutabiri kitakuwaje baadae. Mfano Ukijua gari lina spidi gani kuelekea upande fulani na ukajua acceleration yake, basi unaweza kutabiri kwa uhakika kuwa baada ya muda fulani litakuwa wapi na litakuwa na spidi gani. Samia leo ni raisi inamaana kesho samia atakuwa raisi.
Sasa kama imani hii iko sahihi, ulimwengu ni determined, inamaana tunaishi kwenye Movie. Ukiwa unaangalia movie ukafika katikati ukapause, wale waigizaji mule ndani hawajui movie itaishaje na hawawezi kubadili movie yani inabidi iendelee tu kama ilivyokwisha andaliwa. ingawa wanapoigiza ni kama vile kila wanaloanya wanafanya kwa hiari yao. Unaweza kukuta katikati ya movie anafanya kitu halafu anakuja kukijutia baadae.
Huenda hata haya maisha yameshapangwa sema tu sisi hatujui.
Yani ukiamua ucheke sasa, sio wewe uliyeamua ila ulikuwa umepangiwa kucheka muda huu. Na nadhani wanaoamini kuwa Mungu anajua kesho yetu, inabidi waamini katika hii determinism.
Sasa kama ulimwengu ni determined na kila kitu kimeshapangwa, je sisi tuna free will?
7. Indeterminism: Hii imani ni kinyume cha hiyo deteminism, yaani kwamba ulimwengu hautabiriki ila kila kitu kinatokea randomly by chance. Ulimwengu hauna end-goal au lengo lolote. maisha yanaplay out by chance tu kulingana na hiyo scenario/case husika. Mfano, Samia kuwa raisi haikuwa imepangwa ila ilitokea tu randomly by chance baada ya mkuu wake kufariki. Hakuna mpango au anayepanga chochote ila ni bahati u ndio inatawala ulimwengu...Sasa hata kama ukiamini hii indeterminism, bado tu hakuna free will maana kumbe sio hiari yetu tena bali ni bahati/chance/randomness ndio inaendesha maisha yetu. Sisi hatuna uhuru wa kufanya lolote kwenye haya maisha maana kila kitu kinatokea by chance.
Mimi bado nakuna kichwa sijapata jibu kama binadamu tuna free will au la!
Vipi wewe mkuu, unadhani binadamu tuna free will? Kwanini?
Uhakika Bro