Je, Boniface Mwabukusi atafanikiwa kuirejesha TLS kwenye ubora wake?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nakiri wazi kabisa kwamba baada ya Uongozi wa Fatuma Karume na Tundu Lissu kumalizika , TLS iliuawa, Edward Hosea na Huyu Sungusia ni kama walikuwa Mamluki waliokuja kukiua hicho chama cha Wanasheria, sijui kwanini waliamua kukiua.

Bali sasa Ujio wa Boniface Mwabukusi kwenye uongozi wa Chama hicho ni sawa na Ufufuo na Uzima


Huyu anafahamika kwa utetezi wake kwenye Rasilimali za Nchi, Lakini Je ataweza kufikia viwango vya Karume na Lissu?

PIA SOMA
- Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi imemuengua Boniface Mwabukusi kugombea nafasi ya Rais wa TLS
 
Huyo anataka kupeleka mambo ya siasa hapo wacha tuanze kusaga kunguni!
 
Kazi ya TLS siyo kutetea raslimali za nchi bali jukumu la TLS ni Kuisaidia Serikali na Mahakama kuhusu mambo yoyote yanayogusa sheria, utawala wa sheria na kazi za kisheria. Dhana hii ndiyo inayoiunganisha Taasisi hiyo na Mahakama ya Tanzania.

Kama Mwabukusi ni mwanaharakati basi TLS siyo mahali pake
 
Mwanaharakati maana yake nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…