Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Mwanaharakati ni mdai mabadiliko ya kijamii au kisiasa. Kwa ujumla, anatakiwa afahamu malengo na na tija iliyokusudiwa kupatikana katika harakati hizo.Mwanaharakati maana yake nini?
Lazima awe na imani kamili juu ya anachokipigania kuwa ni haki, imani ambayo itamfikisha katika kiwango cha kumridhisha na kumfanya kuwa na yakini na kuondoa shaka kabisa. Kujitambulisha kuwa mwanaharakati kunahitaji ujuzi kamili wa malengo yaliyokusudiwa, na kisha kujiridhisha wewe mwenyewe na malengo hayo. Lazima mwanaharakati kwanza awe na ujuzi wa itikadi yake.
Kubwa kuliko yote ni kuwa tayari kuyatumikia malengo yenyewe na kubeba dhamana ya matokeo yake yakiwa mazuri au mabaya. Linalojulikana zaidi ni kuwa, kudai haki daima ni mapambano, maana madhalimu siku zote hawako tayari kutoa haki kwa hiyari, mwana falsafa mmoja alipata kusema. “Haki haiombwi, huchukuliwa