Je, Boniface Mwabukusi atafanikiwa kuirejesha TLS kwenye ubora wake?

Mwanaharakati maana yake nini?
Mwanaharakati ni mdai mabadiliko ya kijamii au kisiasa. Kwa ujumla, anatakiwa afahamu malengo na na tija iliyokusudiwa kupatikana katika harakati hizo.
Lazima awe na imani kamili juu ya anachokipigania kuwa ni haki, imani ambayo itamfikisha katika kiwango cha kumridhisha na kumfanya kuwa na yakini na kuondoa shaka kabisa. Kujitambulisha kuwa mwanaharakati kunahitaji ujuzi kamili wa malengo yaliyokusudiwa, na kisha kujiridhisha wewe mwenyewe na malengo hayo. Lazima mwanaharakati kwanza awe na ujuzi wa itikadi yake.
Kubwa kuliko yote ni kuwa tayari kuyatumikia malengo yenyewe na kubeba dhamana ya matokeo yake yakiwa mazuri au mabaya. Linalojulikana zaidi ni kuwa, kudai haki daima ni mapambano, maana madhalimu siku zote hawako tayari kutoa haki kwa hiyari, mwana falsafa mmoja alipata kusema. “Haki haiombwi, huchukuliwa
 
Sidhani kama atapewa maana kwasasa serekali inadhibiti hicho chama kisiwe na kiongozi mwenye misimamo mikali.
 

CCM na serikali wataingilia michakato hiyo ili tu kuhakikisha hapati fursa ya kuongoza taasisi hiyo..

Walifanya hivyo wakati wa Tundu Lissu lakini kwa huyu mwamba (Tundu Lissu) waligonga mwamba kwa sababu TL huwa akiamua na kung'ang'ania jambo au kitu huwa mpaka akipate so long as anakuwa na sifa ya kukipata..

Huyu Bon Mwabukusi kwa karibu namwona ana elements za Tundu Lissu. Ni mpambanaji jasiri asiye mwoga na mpigania haki wa kweli...

Wanachotakiwa TLS ni kumpa support tu kisha mapambano ya serikali/CCM na yeye wamwchie..
 
Uchaguzi wa TLS huwa hauna figisu?
 
Wacha afanye Kwa sehemu Mungu atakayomjalia. Ila Hali ni mbaya Ndio ukweli. Isitoshe Serikali itahakikisha Kwa gharama yeyote hashindi Kwa sababu
haungi mkono wenye mamlaka katika kuchakachua Rasilimali za nchi.
Lingine Mawakili wenzake wengi wamenajisika Hili liko wazi
Mawakili wasomi wote sasa hivi Wanakaa na Majaji/Mahakimu kuangalia mteja mwenye pesa apewe ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…