Je, Bunge Linaidharau Mahakama na Kuwadharau Watanzania? Kitendo cha Bunge Kutunga Sheria Batili Iliyoshabatilishwa na Mahakama Kinamaanisha Nini?

Mayalla, bila shaka wewe ni mkristo, rejea bibli, hiki kiburi sicha kawaida, kina maana kubwa sana sana katika ulimwengu wa "KIROHO", hata haya matamko ya viongozi, " Mawaziri, Wabunge, viongozi wa Chama nk" yaliyojaa " KIBURI" kejeli na dharau, si bahati mbaya, na hawataacha kwani kuna mambo Mungu anayatengeneza kwenye ulimwengu wa "KIROHO", na mwisho yatatokea kwenye ulimwengu wa " KIMWILI" kwa sababu hiyo tutashuhudia mengi zaidi ya haya hebu soma, kukuhakikishia hili soma-: 1 Samwel 2:25.....
 
Paskal asante kwa makala nzuri na elemishi.
Pana tatizo kubwa jinsi ya kutazama na kutafasri mambo kunakopeleka kwenye upotoshaji.
Hukumu za mahakama ni vyanzo vya sheria na havitakiwi kuungwa mkono na bunge- vinasimama vyenyewe. Mahakama kutoa amri na kuliiagiza bunge ni kitendo cha kustajabisha sana- kinaingilia uhuru wa bunge na wala hakina sababu.
 
Utaitwa tena bungeni ukajieleze, kama ulivoitwaga kipindi kile cha ndugai.

Advocate "mayala "
 
Mkuu comte , hiki ulichofanya wewe, ndicho Mahakama ya Rufaa ilichofanya kulikingia Bunge lisiamrishwe na Mahakama.
Bunge limevunja katiba kutunga sheria batili, kisha bunge likavunja katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu, na uchomekeaji wenyewe pia umefanywa kiubatili!. Mahakama Kuu ikatoa amri kuwa sheria hiyo ni batili na mabadiliko ya katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu pia ni batili, hivyo sheria hiyo ni batili, na mabadiliko hayo ni batili serikali urekebishe ubatili huo.

Mahakama ya Rufaa ikalikingia kifua bunge kwa kulishauri lenyewe ndio liuondoe ubatili huo. Kwanini Bunge mpaka leo halijauondoa ubatili huo? Niliuliza Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Nikauliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Pia nikauliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?
P
 
Maelezo mujarabu sala ila kila siku najiuliza ilikuaje mkuu na weledi wako uliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge pale Kawe 😃😃😃ulijibagaza sana mkuu.
 
Uliza vizuri swali lako: ni Mahakama kudharay Bunge, usisahau kuwa Bunge linachaguliwa Mahakama haichaguliwi. Ndiyo maana kukawa na House of Lords na House of Commons - Common people walipochoshwa kunyanyaswa na mabwanyenye. Unless jambo ni la wazi wazi, Bunge liko juu zaidi.
 
Maelezo mujarabu sala ila kila siku najiuliza ilikuaje mkuu na weledi wako uliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge pale Kawe 😃😃😃ulijibagaza sana mkuu.
Ile ilikuwa ni strategia!, ukinisoma hapa utanielewa Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Unapokuwa vitani kuna wapambanaji wa aina mbili, wapambanaji shupavu na wapambanaji makini. Wapambanaji shupavu ni watapambana mpaka mwisho, no matter what,
wao ni watu wa no retreat no surrender watapigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu, hata kama all will be wiped out. Lakini wapambanaji makini, don't fight a loosing battle Elections 2015 - Tuko Vitani Tuna Wapiganaji Shupavu, Wapiganaji Makini na Watazamaji, Je! Wewe Uko Kundi Gani ? mimi niko kundi la wapiganaji makini

P
 
Nilikuwa nasoma kwa umakini wa kutosha ili nione huo ubatili wa sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.
Lakini sijaona ufafanuzi wa ubatili huo.
Rudia kusoma hukumu ya mahakama ya rufaa na utajua ruling yao ilisemaje- huo ndio msingi wa bandiko la mtoa Mada… Bunge waliambiwa wakaoge- wao wananawa na kupangusa pangusa. Kuna tofauti kubwa sana ya kunawa na kuoga. Vifungu batili ni batili tu na cosmetic changes iliyofanyika bado haijatibu tatizo…
Wakati tatizo bado lipo, wanatunga sheria mpya uchaguzi na kujisahaulisha mahakama ya rufaa ilisema wafanye nini…labda watamrejesha mgombea binafsi kama walivyo ambiwa warekebishe…?
 
Nenda mahakamani, hapa unakuwa ni unafiki tu.
Tuliolelewa kwa heshima ya kiasili ya kiafrika, mzazi ni mzazi tuu anatakiwa kuheshimiwa no matter what, unaanzaje kwenda mahakamani kumshitaki mzazi wako?.

Kwa vile Mzazi anakuja kututembelea , nimetafuta wazee nimewaeleza, hivyo akija wazee ndio wamweleze sio sisi watoto. Rais Samia, mgeni rasmi, AGM ya TLS, Wanasheria tumweleze ukweli kuhusu ubatili wa Katiba yetu na sheria zetu, turudishe haki kuu ya Msingi!
P
 
Mara kwa mara tunaandika na kusema CCM ndiye baba wa uovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…