Je, Bunge Linaidharau Mahakama na Kuwadharau Watanzania? Kitendo cha Bunge Kutunga Sheria Batili Iliyoshabatilishwa na Mahakama Kinamaanisha Nini?

Je, Bunge Linaidharau Mahakama na Kuwadharau Watanzania? Kitendo cha Bunge Kutunga Sheria Batili Iliyoshabatilishwa na Mahakama Kinamaanisha Nini?

Mkuu comte , hiki ulichofanya wewe, ndicho Mahakama ya Rufaa ilichofanya kulikingia Bunge lisiamrishwe na Mahakama.
Bunge limevunja katiba kutunga sheria batili, kisha bunge likavunja katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu, na uchomekeaji wenyewe pia umefanywa kiubatili!. Mahakama Kuu ikatoa amri kuwa sheria hiyo ni batili na mabadiliko ya katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu pia ni batili, hivyo sheria hiyo ni batili, na mabadiliko hayo ni batili serikali urekebishe ubatili huo.

Mahakama ya Rufaa ikalikingia kifua bunge kwa kulishauri lenyewe ndio liuondoe ubatili huo. Kwanini Bunge mpaka leo halijauondoa ubatili huo? Niliuliza Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Nikauliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Pia nikauliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?
Paskal, nimekulewa sasa na hapo mwanzo. Bado naendelea kusimama na hoja yangu, Mahakama inatakiwa tu kutoa uamuzi kuwa sheria fulani ni batili na kutuza desturi yake ya kuto mnyooshea yeyote kidole kuwa alikosea. Mahakama hufanya hivyo baina yao kutoka ngaziya chini kwenda ya juu zaidi. Ni nadra kuona mahakama ya juu ikisurubu mahakama ya chini kwa maamuzi yake. Nilitaraijia ustaarabu uwe wa hali ya juu zaidi linapokuja suala linalogusa mihimili weza hasa bunge
 
Heshima ikizidi sana inakuwa ni unyenyekevu, mhimili wa mahakama unajinyenyekeza kwa mhimili wa Bunge na serikali, baada ya mihimili hiyo kuvunja katiba kwa kutunga sheria batili, kisha kuuchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya katiba yetu kiubatili!. Checks and balance itatoka wapi?.
P
 
Bunge aliweza tunga sheria kinyume na katiba.

Lakini bunge pia linaweza badili (kufanya amendments) na kuongeza masharti ya katiba kwa mujibu wa ibara ya 98 na kutunga sheria mpya baada ya hapo.

Sasa issue hapo labda iwe bunge alikufuata amendment process za katiba kwa mujibu wa ibara ya 98, kabla ya kubadili katiba na kutunga hiyo sheria.

Vinginevyo katiba sio fixed inakuwa na utaratibu wa kufanya amendments kawaida hayo mambo yanaelezewa kwenye katiba.
Mkuu Mayor Quimby ,kwanza asante kwa kuchangia uzi huu,na mchango wako ni very objective ila umeharibu hapa
MaCCM hayana desturi ya kuheshimu katiba kwenye kutunga sheria.
Sio fair CCM kuiita maCCM, ni lugha ya maudhi na machukizo。
P
 
Back
Top Bottom