comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Paskal, nimekulewa sasa na hapo mwanzo. Bado naendelea kusimama na hoja yangu, Mahakama inatakiwa tu kutoa uamuzi kuwa sheria fulani ni batili na kutuza desturi yake ya kuto mnyooshea yeyote kidole kuwa alikosea. Mahakama hufanya hivyo baina yao kutoka ngaziya chini kwenda ya juu zaidi. Ni nadra kuona mahakama ya juu ikisurubu mahakama ya chini kwa maamuzi yake. Nilitaraijia ustaarabu uwe wa hali ya juu zaidi linapokuja suala linalogusa mihimili weza hasa bungeMkuu comte , hiki ulichofanya wewe, ndicho Mahakama ya Rufaa ilichofanya kulikingia Bunge lisiamrishwe na Mahakama.
Bunge limevunja katiba kutunga sheria batili, kisha bunge likavunja katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu, na uchomekeaji wenyewe pia umefanywa kiubatili!. Mahakama Kuu ikatoa amri kuwa sheria hiyo ni batili na mabadiliko ya katiba kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu pia ni batili, hivyo sheria hiyo ni batili, na mabadiliko hayo ni batili serikali urekebishe ubatili huo.
Mahakama ya Rufaa ikalikingia kifua bunge kwa kulishauri lenyewe ndio liuondoe ubatili huo. Kwanini Bunge mpaka leo halijauondoa ubatili huo? Niliuliza Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
Nikauliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Pia nikauliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?