Je, CDF na IGP wakifikisha miaka 60 wanaweza kuongezewa muda au lazima wastaafu?

Mabeyo atakuwa na 60+ years

Nilisoma mahali yeye Ni class of 79 monduli amesoma na mwakibolwa mwaka mmoja hapo monduli

Mwakibolwa kashastaafu yeye yupo
Taratibu za maofisa wakubwa wa jeshi na kustaafu zinategemea umekaa katika ngazi fulani kwa miaka mingapi, na ukashindwa kupanda cheo kifuatacho kwa sababu umeshindwa kupita mitihani ya kukupandisha. Hii ndiyo inatokea unakuta vijana wadogo tu kwenye ngazi za major, Lt. Colonel na Makanali wanastaafu kabla ya kufika miaka ya kustaafu ile ya uraiani. Ingawaje sikumbuki kikamilifu ni miaka mingapi, lakini unatakiwa kukaa kwenye ngazi miaka fulani, usipopanda unapumzika (unastaafu).
 
Sahihisho: RPC siyo ngazi/cheo cha polisi, bali nafasi ya kiutawala. Inawezekana alikuwa RPC lakini mwenye cheo kikubwa. Kumbuka wakuu wote wa police wa mkoa hawalingani vyeo. Kuna wengine ni Commissioners, Deputy Commissioners, Senior Assistant Commissioners, Assistant Commissioners, na kuna wakati hata Senior Superintendents wanakuwa RPC. Mahita anaweza kuwa alikuwa na cheo kikubwa kipolice lakini ni RPC.
 
Sio lazima rais kushauriana na mtu yeyote katiba inampa mamlaka rais kufanya anavyoona yeye yaani rais akae na mamejor general ashauriane nao kuhusu uteizi wa cdf uliona wapi hiyo
Theoretically uko sahihi lakini pia inaonekana hujui kuwa rais hupata ushauri kutoka jeshini kabla ya kuteua majenerali hata kama katiba inamruhusu; hata wakati anampandisha Mbuge papo kwa papo pale Dodoma bado alikiri hadharanai kuwa tayari alishashauriana na uongozi wa jeshi. Zamani ilikuwa ni rahisi kufanya hivyo lakini sasa jeshi limeshakuwa kubwa sana na kuna transparency kubwa kiasi kuwa Rais hawezi kujiamulia kumteua kamanda bila kuwa na support ya jeshi.

Sikiliza hotuba hii vizuri jinsi anavyoianza

 

Kwa miaka ya sasa ambayo watu wamekwenda mafunzo mbalimbali ya kijeshi na kiutawala, mtu akichafika cheo cha kanali au brigedia ana uwezo wa kushika vyeo vyovyote vilivyobakia vya kijeshi na kwa ufanisi mzuri tu. Vyeo vilivyobaki vinarudiarudia mambo yaleyale ya kiutawala, tofauti kubwa ni scale.
 
Sidhani Kama hii Ina apply Tanzania

Labda marekani

Huku mbona tunawaona wazee Wana staafu maluteni na makapteni
 
Sahihi kabisaaaa...
 
Unapoteza kumbukumbu magu amekwenda kuwavisha nishani monduli mwaka 2016 kuwavisha nishani nje ya monduli ni maamuzi yake kama rais
Siyo Monduli bali uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
 
RCO wenye vyeo vya ssp ni wengi tu..RTO ndio unawakuta mpaka ASP kutegemea na ukubwa wa mkoa husika.
 
General Mboma alipopandishwa cheo kuwa General na kuwa CDF hakuwa Lt. General bali alikuwa Major General. Aliwaruka wengi waliokuwa senior wake aliwemo Lt. General Martin Mwakalindile ambaye baadaye alipepelekwa Maputo Mozambique kuwa balozi.
 
Kama ilivyo sasa kati ya Sirro na Mambo sasa, kuna clip Sirro anamnanga hadharani kabisa...
 
Pengine mazoea tu na tabia za watu

Ila afisa JWTZ maslahi manono sana hamna wa kuwalinganisha serikalini
Mbona ndugu yangu mmoja alistaafu akiwa na nyota 3 lakini alikuwa kawaida sana, hata gari hakuwa nalo?? Nyumba ya kawaida sana tuu
 
Mbona ndugu yangu mmoja alistaafu akiwa na nyota 3 lakini alikuwa kawaida sana, hata gari hakuwa nalo?? Nyumba ya kawaida sana tuu
Hakuwa bloodie huyo angekuambia vizuri maslahi yake ,mbona hata vyuo mishahara mikubwa mikubwa lakini wanastaafu wanapanda daladala

Ingekuwa mmoja ameoa afisa JWTZ labda akawa anatoa info ndio watu wangeelewa sema ishu za viapo vya usiri wa kazi za jeshi , uafisa wa jeshi unaambatana na umahiri wa usiri mkubwa

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…