Je chadema kutoweka ukomo wa kugombea nafasi ya uongozi walikosea?

Je chadema kutoweka ukomo wa kugombea nafasi ya uongozi walikosea?

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2020
Posts
400
Reaction score
484
Salaam wana Jamvi,ninavwatakieni jumapili njema yenye baraka tele.baada ya kusema hivo,hebu nirudi kwenye mada yangu.kumekuwa na shinikizo kubwa sana la watu kutaka chadema wa badilishe kifungu kwenye katiba Yao kina cho ruhusu mtu kugombea nafasi yoyote bila ukomo mpaka wanachama watakaposema inatosha sasa.kuna upande wawanataka mabadiliko hayo wametoa hoja kadha wakisema
1,mtu akikaa sana madarakani ujenga imaya ya machawa
2.anaizoea nafasi na kujenga tabia za kidikteta.
3.ili kuimarisha na kuboresha chama ni muhimu kuleta damu mpya na akili yenye mipango mipya nk
Wametoa sababu nyingine nyingi zenye mashiko.sasa turudi kwenye swali langu ,je chadema kutoweka ukomo wakugombea nafasi ya uongozi walikosea?.kwanza nilazima tukubaliane kwamba suala lakuandika katiba ni suala la kitaalam.ambalo Lina hitaji watu wenye uwezo wakitaluma kuweza kuianda,kushauri,kuelimisha mpaka kuandika katiba yenyewe.kwa upande wa wataalam wa hiyo taluma chadema wanabahati ya kuwa na magwiji wa Sheria wa kiongozwa na makamu mwenyekiti wao mh tundu antipas lissu .inasemekana kuwa wakati wanafanya mabadiliko ,ikiwemo kuondoa ukomo wa uongozi mh lissu ndiye aliyekuwa mwanasheria mkuu wa chadema.kwa maana hiyo yeye ndiye aliyekuwa mshauri mkuu juu ya faida na hasara ya mabadiliko yaliyofanywa kwenye katiba ikiwemo Hilo la kuondoa ukomo wa uongozi .si na shaka hata kidogo juu ya uwezo wa mh lissu linapokuja suala linalo husu mambo ya sheria.kuhusu chadema kuondoa ukomo wa madaraka naona mwanasheria aliona mbali sana,kwa kuzingatia siasa za vyama vya siasa barani afrika.hususan kwenye uadilifu wakiongozi,uajibikaji,uwezo wa kuhimili siasa za upinzani,ushawishi,msimamo nk .ndio maana mwanasheria akashauri waondoe ukomo,lakini kuwe na kipimo cha miaka mitano.kwamba Kila BAADA ya miaka mitano kiongozi husika atafanyiwa tathmini iwapo ANAfaa au la.ikiwa wanachama wataona ANAfaa watamuongezea miaka mwingine mitano,wakiona hafai watamuondoa na kumchagua mtu mwingine awaongoze.kwa mtizamo wangu Mimi naona kama hawakukosea kuondoa ukomo maana walikumbuka kuweka KIPINDI cha miaka mitano kupima uongozi wa mtu.je mwenzangu unalionaje karibu tujadili kwa ustaarabu.nawasilisha.
 
Back
Top Bottom