Je CHADEMA nao kuchagua Mgombea Urais na Mgombea Mwenza baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti?

Je CHADEMA nao kuchagua Mgombea Urais na Mgombea Mwenza baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti?

Unafahamu uwezo ,mamlaka,nguvu,madaraka na nguvu iliyowekwa mikononi mwa mkutano Mkuu wa CCM Taifa kwa kushirikiana na kamati kuu na halmshauri kuu? Hapo vyombo vyote vya maamuzi vilikuwepo na Ndivyo vilivyofanywa maamuzi.

Kwa hiyo Embu acha kuendeleza umbumbumbu wako na ujinga.
Wewe ni mjinga! Kwakua simfahamu iweke na uoneshe kwamba Kuna kikundi Cha watu wachache katika chama ambacho kina nguvu kuliko wanachama wenyewe? Haya baisnisha kama nilivyoonesha mkutano na vikao vilifanyika lini?
 
Kama Mimi nimesoma katiba Haina maana kwamba Kila mtu huku ameisoma! Nakufundisha tena unapoleta hoja Ili usionekane Kwamba ni UWT pro! Unafaa ushikamanishe hoja Yako na reference!
Umesoma hiyo ibara ya 47(3)? Umeielewa? Akili zimekurudi?😀😀
 
Umepata posho za mkutano mkuu au hakuna anae kujua kordo za lumumba?
 
Wanaweza, kama ccm wamefanya surprise kwenye mkutano wao, chadema itashindwaje? Tulia upate majibu murua
 
Ndugu zangu Watanzania,

CCM ni chama kiongozi Barani Afrika na ndicho chama ambacho hutoa Dira na mstakabali wa Taifa hili. Ambapo mambo yake mengi yamekuwa kama Dira na muelekeo wa Taifa hili.

Lakini pia vitu vingi sana ambavyo vimekuwa vikifanywa na CCM vimekuwa vikiigwa sana na vyama vya upinzani hapa Nchini na hata nje ya Nchi.ndio maana na sababu ya kuona vyama vingi kutoka nje ya Nchi huleta viongozi wake hapa Nchini kuja kujifunza kwa CCM.

Sasa hapo majuzi CCM kupitia Mkutano Mkuu wake maalumu imeweza kufanya jambo la kihistoria kwa kuchagua na kumpitisha Rais Samia kuwa Mgombea wake katika uchaguzi Mkuu ujao mwishoni mwa Mwaka huu.

Ambapo ni katika hatua hiyo imeshuhudia pia Rais Samia akimpendekeza Balozi DKT Emmanueli Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wake.Hii ni baada ya dkt Philipo Isdori Mpango kuomba kupumzika .

Sasa kwa kuwa upande wa pili wa upinzani kwa chama kikuu cha Upinzani kuna wakutanisha wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho na wajumbe wengine mbalimbali wapo jijini Dar es salaam kwa sasa katika kumchagua mwenyeketi na makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

Nilikuwa nauliza je CHADEMA Nao wanaweza wakamaliza shuguli hiyo hii leo? Je na wao wanaweza kuamua kupunguza kazi ya siku za mbele kwa kumpitisha mgombea Urais na mgombea Mwenza hii hii leo?

Ikumbukwe ya kuwa CHADEMA imekuwa ikiiga mambo mengi sana kutoka CCM.lakini pia imekuwa ikiangalia upepo wa CCM. Au wanasubiri mgombea kutoka CCM aende kwao na wampatie kugombea Urais.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Siku nyingine ukipost thred sindikiza na kapicha kako tukikuona ukibubujikwa na michozi ya furaha na kulia kwa kwikwi huku ukigalagala chini
 
Back
Top Bottom