Je, chemchem ya maji ya Kilimanjaro ni Kweli au Propaganda za Masoko?

Je, chemchem ya maji ya Kilimanjaro ni Kweli au Propaganda za Masoko?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Kwanza kabsa; uzi huu hauna maana yoyote ya kuharibu biashara zozote za Makampuni ya Bonite pamoja na Azura.

Kwenye biashara mitaa bhana siku hizi kuna simulizi zinazosisimua: tone la mvua linasafiri kwa miaka 20 ndani ya miamba ya Mlima Kilimanjaro, likichujwa kiasili hadi kufikia kitalu cha maji (aquifer) futi zaidi ya 400 ardhini. Kutoka Azura hadi Kilimanjaro Drinking Water, simulizi ni ile ile—maji "yasiyoguswa na mkono wa binadamu." Lakini je, tunakunywa baraka za mlima mrefu kuliko yote Afrika, au tunakunywa mbinu bora ya masoko?
images - 2026-01-22T200245.574.jpeg

Wataalamu wa jiolojia wanahoji: Je, inawezekana kitalu kimoja cha maji kitoe mabilioni ya lita kwa makampuni tofauti bila kupungua?
images - 2026-01-22T200326.517.jpeg

Wakati chapa hizi zikijivunia "asili ya mlimani," ukweli ni kwamba visima vingi viko mitaa kadhaa pembezoni mwa mlima na si ndani ya hifadhi yenyewe.
drinking-water-on-kilimanjaro-2-400.webp

Kijiolojia, maji yanayotiririka kutoka Kilimanjaro husafiri kupitia mifereji ya chini ya ardhi (subterranean channels). Kampuni inaweza kuchimba kisima kilomita 20-30 kutoka mlimani na bado ikadai kitaalamu kuwa maji hayo yanatoka kwenye "mfumo wa mlima huu."
images - 2026-01-22T200637.724.jpeg

Kisheria, kampuni inaweza kutumia jina la eneo ikiwa maji yanatoka kwenye bonde la mto husika, hata kama kiwanda kiko mbali na kilele cha Kibo. Hapa ndipo penye utata; je, ni maji ya mlima au ni maji ya mfumo wa kawaida wa ardhi yaliyopambwa kwa picha ya mlima Kilimanjaro?
shutterstock_1073808692-1.jpg

Hapa mtumiaji anabaki njia panda: Je, unalipia maji ya kunywa ya kipekee, au unalipia hadithi nzuri iliyochapishwa kwenye chupa ya plastiki?
 
unalipia hadith nzuri iliyochapishwa kwenye chupa ya plastic mkuu, ningeongea zaid ila sitaki kuharibu biashara za watu mkuu
 
Kwanza maji ya chemchem za kilimanjaro ni bora kuliko hizo takataka za kwenye chupa , pili maji haya kuisha ni ngumu , yamelea maelfu ya vizazi vyetu tangu enzi na enzi.
 
Kiuhalisia hayo maji si yale yanayotiririka toka juu ya mlima kilimanjaro, hayo ni maji mengine kabisa nje ya mlima kilimanjaro. Wapo wengine nao wanaji brand kwa milima ya usambara, uluguru, kipengere na kwingine kunako sisimua wateja. Hizo ni strategy tu za kibiashara
 
Songea, njombe, iringa Kuna Maji wanasema nayo ya kutoka hifadhi ya kitulo kama sijakosea Maji wanaita kitulo
Bongo mambo ni mengi sana
 
Back
Top Bottom