Je, daktari katika kesi ya mauaji alipokea rushwa au nayeye alikuwa na matatizo ya akili alipotoa ripoti mbili kinzani mahakamani?

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Kuna kitu ambacho siyo cha kawaida kwenye kesi inayomkabili bwana Hamis Luwongo aliyehukumiwa jana na mahakama ya kuu ya kanda ya Dar es salaam kwa kosa la kumuua mkewe kisha kuuchoma moto mwili wa mkewe.

Katika kuhakikisha inatenda haki, mahakama iliomba mtuhumiwa afanyiwe vipimo vya akili.

Issue inaanzia hapo.
Bwana Luwongo alifanyiwa vipimo vya akili na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili Dk. Sadiki Mandari, kutoka hospitali ya taifa ya afya ya akili Mirembe.

Cha kushangaza ni kwamba ripoti ya kwanza aliyo present mahakamani inasoma kuwa mtuhumiwa bwana Luwongo alikuwa na matatizo ya akili. Ikabidi mahakama imuite daktari aje atoe ushaidi huo mahakamani.

Cha kushangaza, Dk. Mandari alipokuja mahakamani aliwasilisha ripoti kinzani na ile ya kwanza kitendo ambacho kilimkasirisha Jaji Mwanga.

Je, ni sahihi Jaji Mwanga kuishia kukasirika, au Dr. Mandari awajinishwe 1). Kwa kuidanganya mahakama; 2). Kukiuka maadili ya kazi?

 

Attachments

  • IMG_1579.png
    543.5 KB · Views: 3
Hii dunia ina watu jamani. Hivi huyo daktari angekuwa huyo aliyeuwawa ni mwanae halafu aambiwe amchunguze bwana Luwongo angeandika ripoti kama hiyo kweli? Inatia hasira sana. Siku hizi watendaji waadilifu wanazidi kupunguwa matokeo yake watu wasio na uwezo wanadhulumiwa haki zao. Kwa mauaji yale ya kikatili halafu jamaa lilivyo na roho ngumu linamchoma mkewe kama ndafu halafu bado anatokea mtu anayetegemewa na jamii kutokana na taaluma yake adhimu anataka kumchomoa huyo muuwaji hii si sawa kabisa.
 
System ya afya ndivyo ilivyo! Kuna zile fomu za medical report...madaktari wengi wanajaza hata wakiwa bar!
Fomu inahitaji uchunguzi lakini inaanfikwa NAD na NIL za kutosha!
Inaonekana akili za Daktari xilirudu alipo pokea wito wa kutetea ripoti yake mahakamani!

Kifupi kada nyingi wanatumia BAU principle kwenye utendaji! Hata huko huko mahakamani!
 
Sasa ndugu watu wanafanya kazi wapate fedha waishi vizuri. Utakuwaje mwadilifu wakati wanasiasa na viongozi nao wanapiga kwa nafasi zao?
Ulitaka Daktari aache huo mpunga?
We huoni mitaani Mwl Nyerere anavyochekwa kwa kuiacha familia yake ikiwa haina mali na fedha?
Watu wapo kimaslahi na fedha! Jamii itajijua yenyewe. Hapo ndipo ccm ilipotufikisha!

NB: huyo bwana aliyemuua mkewe na Daktari pia wote wana changamoto ya afya ya akili.
Msiuane. Kama mmechokana achaneni tu! Kinachokufa ni mwili, roho haifi!
 
Au hiyo report iliyowasilishwa mahakamani awali ilichakachuliwa!
 
HUyu WA kuhiji wasimwachie
 
Tungeanza na DPP
 
Hivi ndivyo madaktari wa Tanzania walivyo.Kwa ambao hawawajui huwa wanawaona kwa nje madaktari ni wasafi ila mimi nawajua madaktari kwa ndani ni wachafu.

Madaktari waliwahi kuiaminisha ngazi ya maamuzi uongo kuhusu mimi ili ngazi hiyo ya maamuzi iamue kama wanavyotaka wao,nikadhulumiwa haki yangu.

Lakini Mungu si Dk D..........n wala Mungu si Prof. P...........e , Mwenyezi-Mungu alinifungulia njia nyingine ya kutoboa maisha, Mwenyezi-Mungu alinipeleka mahali pengine penye vinono na pesa ndefu kuliko udaktari.
 
Huenda dr. hakupewa kile alicho ahidiwa akaona bora akachome moto kambi.
 
Mhimu amefungwa, kuua mtu ni kitendo kibaya sn hakuna cha kumtetea huyu naye anapaswa auwawe
 
Wengi ni wajinga haswa
 
HAPO NDIPO UTAELEWA SIO KILA KESI YA KUBAKWA N HALALI WENGINE MA DK HULA RUSHWA
 
Kila mtu ana matatizo ya akili, hata wewe mtoa mada, tunatofautiana kiwango tu, hata ulalamishi kama wa mtoa mada ni matatizo ya akili
 
Huyo muuaji ana kiburi, majivuno, hautii, kiufupi ni mshenzi, anapaswa anyongwe haraka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…