Watu walipokuwa wanaongelea demokrasia watu hawakuelewa wengine , demokrasia ikibakwa kwa wapinzani baadaye huhamia ndani ya chama tawala. Uamuzi wa kufanya anavyotaka kwenye serikali za mitaa ndio uliokuwa unafanya alazimishe madiwani wote wawe wa kwake.
Ni wazi kungekuwa kuna madiwani wa vyama vingi barazani hangethubutu kufanya hivyo kwakuwa malalamiko yangekuwa mengi, kama tu wakati ule kuweka meya wake alikuwa anashindwa, kwa kuhofia vurugu Leo sasa ccm wameona huyu mtu alivyokuwa na dharau. Unavunja halmashauri hata bila kushauriana na meya wahusika. Dharau sana, anajua hawana la kumfanya na hawana pa kwenda kulalamika au kungekua na wapinzani barazani wangeungana nao ,hawapo.
Na huu ni mwanzo tu wa uvunjaji wa demokrasia ndani ya chama chake mwenyewe. Hata mkapa alipovunja halmashauri hakukurupuka alifanya utafiti na aliwashirikisha un-habitat.
Watu wanasema hata mameya hawaheshimiki tena anawaona kama madiwani tu. Mnaona hata alivyomtukana meya wa morogoro hadharani. Unajua mtu akikupa kitu bure lazima akusimange. Kama pia wabunge wanavyosimangwa bila magufuli hawangefika bungeni hivyo wafunge midomo