Je, Dar es Salaam watu wamekubaliana kukaa nyumbani?

Je, Dar es Salaam watu wamekubaliana kukaa nyumbani?

BMWsimba

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
347
Reaction score
512
Leo nimekaa kituo cha Makumbsho magari ya posta mda WA asubuhi huwa kuna kuwaga na abiria wengi sana saa 7:00 mpka saa 8:00 asubuhi sijaona watu wakiwa wengi kama kawaida, nimepita barabara ya new Bagamoyo road mpaka Morocco magari sio mengi na hamna foleni Ile ya asubuhi hata trafiki hakuwa anaongoza magari ameachia taa zifanye kazi yake maana Kwa kawaida asubuhi wanakuwa wanaita magari yanayotoka mwenge kuja katikati ya jiji.

Hivyo na mataa ya salenda taa zinaongoza magari na hamna foleni, kidgo ni mataa ya kinondoni kuna changamoto sababu barabara ni nyingi na kuna hitaji Askari WA kuweza kubalance hapa kuna trafiki pamoja na dar free market, masaki yote nimezunguka hakuna foleni za magari na kuna magari machache kama upo nje ya mji kabisa, posta Samora ndo nipo hapa hakuna misururu ya magari kama ilivyokawaida, bila kusahau mataa ya nmb hq na maktaba bibititi rd yote yanajiongoza na hakuna foleni....

Nadhani mpaka ijumaa Sisi wafanyabiashara wa Uber tutataanza rudisha magari kwa mabosi maana hata gari za Uber zilizokuwa zinajaza foleni hazionekani Mungu atusaidie Tu. Kama Una hela zako ni wakati wa kutumia kwa uangalifu na kuwa na Akiba ya chakula, na kujiandaa kuuziwa vitu kama viwanja, nyumba, magari, pikipiki, TV, redio, vitanda Kwa bei ya kutupwa maana kitakachokuwa na thamani ni bidhaa ya chakula Tu,

Pia huu sio wakati mzuri wa kufungua biashara mpya, nawatakia asubuhi njema....nipo na tafakari niuze gari yangu ya Uber (IST no DAA) sijui kama nitapata m 8 nimwachie MTU chapu niende kijijini nikapumzike huko Mtwara.
 
Bro kuwa serious kidogo. Yaani IST naomba DAA uiuze mil 8 kipindi hiki? Au imetembea kilomita efu ishirini tu? Acha masihara, juzi tu jamaa anauza IST namba DQR imetembea km kama elfu 60 kwa mil7
Mkuu, IST haijawahi kushuka sana bei uliyonunulia Ila Kwa kipindi Nina wasiwasi Hali inaweza kuwa mbaya zaidi, nikajua kosa mteja wake, maana nataka nihamie kwenye biashara nyingine baada ya korona
 
Mkuu, IST haijawahi kushuka sana bei uliyonunulia Ila Kwa kipindi Nina wasiwasi Hali inaweza kuwa mbaya zaidi, nikajua kosa mteja wake, maana nataka nihamie kwenye biashara nyingine baada ya korona
Tena kama una mpango wa kuuza Fanya fasta kabla mzee korona hajachanganya. Mimi nasubiria daladala za mil kumi tu
 
Tena kama una mpango wa kuuza Fanya fasta kabla mzee korona hajachanganya. Mimi nasubiria daladala za mil kumi tu
Hahahhah we daladala haitopita mwezi maana mengi yameegesha na wiki hii itakuwa mara mbili zaidi maana mabosi wengi walikuwa wanaringa kupokea hesabu pungufu ya asilimia 30 Ila Kwa SASA hata hiyo 30 haipatikani madereva wanataka pungufu ya silimia 50 na wengine kitakachopatikana tugawane
 
Tumeambiwa tufanye kazi na kuchukua tahadhari. Tahadhari ni pamoja na kuacha au kupunguza kusafiri na kubaki nyumbani.

Watu wamejiongeza. Tusisubiri amri ya serikali. Baadhi ya waajiri wamesha amrisha wafanyakazi wao kubaki kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, IST haijawahi kushuka sana bei uliyonunulia Ila Kwa kipindi Nina wasiwasi Hali inaweza kuwa mbaya zaidi, nikajua kosa mteja wake, maana nataka nihamie kwenye biashara nyingine baada ya korona
Juzi j'mosi jamaa kauza IST DM.. 7.5mil, kama gari ina hali nzuri inauzika tu. Wasikutishe.
 
Back
Top Bottom