- Source #1
- View Source #1
Mitandaoni kuna madai ya baadhi ya wauzaji wa dawa za asili kwamba bidhaa zao zinaweza kuti
bu na kuponya kisukari kabisa, hata ndani ya muda mfupi. Kwa mfano, baadhi ya matangazo yanadai kuwa dawa fulani ya asili inaweza kumaliza kisukari ndani ya siku 90. Je, madai haya yana ushahidi wa kutosha wa kisayansi.
bu na kuponya kisukari kabisa, hata ndani ya muda mfupi. Kwa mfano, baadhi ya matangazo yanadai kuwa dawa fulani ya asili inaweza kumaliza kisukari ndani ya siku 90. Je, madai haya yana ushahidi wa kutosha wa kisayansi.
- Tunachokijua
- Ugonjwa wa kisukari ni tatizo la kudumu la kimfumo na ki-metaboliki linaloathiri namna mwili unavyotumia sukari (glucose) kwenye damu . Hutokea pale kongosho linaposhindwa kuzalisha homoni ya insulini kabisa (Aina ya 1), au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri insulini inayozalishwa (Aina ya 2).
Baadhi ya tafiti za kisayansi ikiwemo tafiti za kisayansi zilizochapishwa kitaalamu, hakuna ugunduzi wa kisayansi duniani unaonyesha uwepo wa dawa ya hospitali au ya asili inayoweza kuponesha kabisa na kuondoa ugonjwa wa kisukari mwilini, bali kuna mbinu za kukidhibiti tu ili mgonjwa aishi maisha salama.
Wafanyabiashara wengi wa mitishamba kwenye mitandao ya kijamii kama mitandao ya kijamii kama Facebook, TikTok na WhatsApp wanadai kuwa wana dawa za asili zenye uwezo wa kutibu na kuondoa kisukari kabisa ndani ya siku chache. Mara nyingi wanadai kuwa bidhaa zao zinafufua kongosho lililokufa na kumfanya mgonjwa aache kabisa kutumia sindano za insulini au vidonge vya hospitali.
Matangazo haya husindikizwa na ushuhuda wa video au picha za watu wanaodai kupona kabisa ili kuvuta wateja wenye hofu.Mfano wa madai kama hayo unaonekana katika tangazo la Diabeze Natural, ambalo linadai dawa hiyo huanza kuonyesha matokeo ndani ya siku 3–7 na inaweza kutibu kisukari. Pia, tangazo hilo linadai kuwa dawa hiyo husaidia kurejesha kazi ya kongosho na uzalishaji wa insulini.
Uhalisia wa madai hayo
Uchunguzi wa kina wa kitabibu unaonyesha kuwa baadhi ya mimea ya asili kama mdalasini, tangawizi, mlonge, na aloe vera ina viambata hai vinavyoweza kusaidia kushusha viwango vya sukari kwenye damu. Ripoti kutoka National Center for Biotechnology Information (NCBI) zinabainisha kuwa mimea hii huongeza hisia za seli kwa insulini ili kuruhusu sukari kuingia mwilini kuzalisha nguvu.
Hata hivyo, makala za kitaaluma ikiwemo ya Medical News Today zinabainisha wazi kuwa ingawa mitishamba hii inasaidia, lakini haina uwezo wa kurekebisha uharibifu wa kudumu uliotokea kwenye kongosho au kubadili vinasaba vinavyosababisha ugonjwa huo.
Madai haya si ya kweli na Kulingana na tafiti za kisayansi zilizochapishwa kitaalamu, hakuna ugunduzi wa kisayansi duniani unaonyesha uwepo wa dawa ya hospitali au ya asili inayoweza kuponesha kabisa na kuondoa ugonjwa wa kisukari mwilini, bali kuna mbinu za kukidhibiti tu ili mgonjwa aishi maisha salama.
Miongozo ya kiudhibiti kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inasisitiza kuwa dawa nyingi zinazouzwa mitandaoni hazijapita kwenye mifumo rasmi ya udhibiti na usajili, hazina vipimo sahihi vya dozi, na zinaweza kusababisha sumu inayoharibu figo na ini.
Mwongozo wa matibabu kutoka NKCH Health Blog unaonya kuwa wagonjwa wengi huacha dawa za hospitali baada ya kuamini matangazo haya, jambo linalosababisha sukari kupanda kwa kasi na kuleta madhara ya upofu, kiharusi, au kifo.