Je dawa za kupunguza unene zinaweza kusababisha matatizo ya uzazi?

Je dawa za kupunguza unene zinaweza kusababisha matatizo ya uzazi?

nakula jioni tu ila msosi wa hataree.situmii dawa yoyote mkuu.kutembea siwezi jua kali

Jirekebishe hapo unapokula jioni tu tena umesema mlo wa hatari hapo ndo penye changamoto @ Dada! Mimi nakushauri usikose kupata kifungua kinywa kisha mchana kula kidogo halafu usiku usile kabisa uone Kama hutapata matokeo makubwa sasa (BRN) usiku usile chochote kabisa! Never skip breakfast !
 
Angalizo: swala la kutaka kupungua uzito linahitaji kufanya maamuzi magumu , ujikane , uamue toka Moyoni Mwako na akili yako ijue na kukubali kuwa lazima kupungua uzito! Chukia kula kula , epuka kwenda sehemu zenye vyakula ushawishi wa Watu kutaka ule ule hovyo ! Weka nia !
 
nimefanya jitihada za kujipunguza uzito ila naona nimeshindwa nazidi tu kuongezeka siku baada ya siku.wenzangu wakiongeza mahela mimi naona naongeza kilo.
mazoezi nafanya kidogo naacha naona uvivu
chakula naacha najikuta nimerudia tena tuseme ukweli jamani hakuna asiependa vitu vitamu .nitakula malimao mpaka lini? ni adhabu kuishi kwa diet acheni tu .
natamani kutumia madawa ya kupunguza uzito ila naogopa yasije yakaniathiri mfumo wangu wa uzazi.
naombeni ushauri haya madawa ya kupunguza mwili yana shida yoyote kwenye uzazi?
asanteni
kama uko serias niinbox...nilikuwa mnene pia
 
Mimi nikupe ushuhuda wangu miezi miwili ilopita nilikuwa Na uzito wa wastani wa 70 - 75 kg lakini leo nimepita 56 kg lakini shughuli Yake si ya kitoto, Na bado napambana haswa ! Yani baada ya muda itabidi nifanye shopping ya Nguo zote ! Nakutia moyo inawezekana kupungua ukiweka nia! Lakini mwenzio shuhuli yangu ni kula Matango tena nikikupa formula utashangaa
 
Hii miili tunatofautiana mwingine hata akiwa obesity haimsumbui lakini mwingine akizidi kilo mbili tatu Kwenye BMI Yake ni changamoto mathalani kuwa goigoi, kusinzia hata Ofisini , kuchokachoka n.k wengine dalili za magonjwa n.k
 
Mimi nikupe ushuhuda wangu miezi miwili ilopita nilikuwa Na uzito wa wastani wa 70 - 75 kg lakini leo nimepita 56 kg lakini shughuli Yake si ya kitoto, Na bado napambana haswa ! Yani baada ya muda itabidi nifanye shopping ya Nguo zote ! Nakutia moyo inawezekana kupungua ukiweka nia! Lakini mwenzio shuhuli yangu ni kula Matango tena nikikupa formula utashangaa
Naomba uiweke kama unaweza
 
NEW DIET IN TOWN!
Jaribu hii diet haikunyimi sana...



1.Diet hii kwa siku za mwanzo zile 17 huruhusiwi kula wanga wa aina yoyote.Ugali,wali,ndizi,viazi,chips,pilau,biriani,chapati,maandazi,mikate,mihogo,bitumbua n.k hata kula kimoyomoyo hairuhusiwi.


2.Huruhusiwi sukari ya aina yoyote wala vinywaji vyenye sukari.Soda ni marufuku,juice za mabox hata ukitengeneza mwenyewe huruhusiwi.Pombe hairuhusiwi bia sijui wine or whisky vyote haviruhusiwi.


3.Mafuta hayaruhusiwi mafuta yanayoruhusiwa ni olive oil pekee mafuta ya mzaituni.


4.Hairuhusiwi kula late baada ya saa mbili usiku.Saa mbili ikukute unakula or umemaliza kula.

5.Huruhusiwi kushinda njaa.

6.Hii ni diet inayoruhusu vyakula vya protine na mboga mboga,matunda maalum sio kila tunda.

7.Mayai kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi mawili.Kwa kuchemsha au kukaanga.Ruksa kula ule ute kuliko kiini.Iwapo utakula viini visizidi vinne kwa wiki.Maana mayai yanacolestral ndio maana yana limit.


8.Samaki na kuku iwe kuchoma au kuchemshwa ndio anaruhusiwa kama mlo wa mchana au usiku.


9.Ukitaka kusnack kwenye saa tano au saa kumi tunakula yogurt tena ile ya asas ambayo ni low fat na sio tamu haina sukari ni plain.

10.Kusnack pia unakula matunda kama vile aple,chungwa,matunda jamii ya zabibu,jamii ya baries na mapeasi.Matunda haya yamechaguliwa mwanzoni kwani yanasaidia sana kuboost metabolism ili chakula kuyeyushwe haraka tumboni.Pia yana kiwango kidogo cha sukari.

11..Alfajiri ukiamka unakunywa kikombe cha maji ya moto yenye limao.Yanasaisia kurahisisha mmeng'enyo aa chakula kwa siku hiyo.


12.Kila baada ya mlo utakuwa green tea haya ni majani ya chai yale ya kijani sio meusi.Inamaana kwa siku vikombe vitatu asubuhi,mchana na usiku.

13.Hakikisha unakunywa maji sio chini ya lita 2 kwa siku maji yanasaidia sana kupunguza weight na pia husikii njaaa ukiyanywa ipasavyo.

MANUNUZI
1.green tea
2.yogurt zile za asas plain ambazo hazina sukari na ni low fat.
3.Matunda machungwa,peasi,zabibu,grape fruit,barries zile za aina zote.
4.Mafuta ya kupikia ya olive oil
5.Mayai
6.Samaki
7.Kuku mimi hununua vile vidari ambavyo vishawekwa kwenye kipakti kimoja zinakaa 6.

8.Mboga za majani aina zooote unazozijua wewe.

9.Limao au ndimu
 
Kama kwenye picha hapo ndivyo ulivyo Mis Natafuta mbona wewe mtoto Mashaalah..
 
Swahiba kila la kheri.

Kumbuka sharing is Caring.
Hilo usijali swahiba... najua wazi kabisa kizuri mtu hula na nduguye

_90835278_mediaitem90834547.jpg
 
Back
Top Bottom