NEW DIET IN TOWN!
Jaribu hii diet haikunyimi sana...
1.Diet hii kwa siku za mwanzo zile 17 huruhusiwi kula wanga wa aina yoyote.Ugali,wali,ndizi,viazi,chips,pilau,biriani,chapati,maandazi,mikate,mihogo,bitumbua n.k hata kula kimoyomoyo hairuhusiwi.
2.Huruhusiwi sukari ya aina yoyote wala vinywaji vyenye sukari.Soda ni marufuku,juice za mabox hata ukitengeneza mwenyewe huruhusiwi.Pombe hairuhusiwi bia sijui wine or whisky vyote haviruhusiwi.
3.Mafuta hayaruhusiwi mafuta yanayoruhusiwa ni olive oil pekee mafuta ya mzaituni.
4.Hairuhusiwi kula late baada ya saa mbili usiku.Saa mbili ikukute unakula or umemaliza kula.
5.Huruhusiwi kushinda njaa.
6.Hii ni diet inayoruhusu vyakula vya protine na mboga mboga,matunda maalum sio kila tunda.
7.Mayai kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi mawili.Kwa kuchemsha au kukaanga.Ruksa kula ule ute kuliko kiini.Iwapo utakula viini visizidi vinne kwa wiki.Maana mayai yanacolestral ndio maana yana limit.
8.Samaki na kuku iwe kuchoma au kuchemshwa ndio anaruhusiwa kama mlo wa mchana au usiku.
9.Ukitaka kusnack kwenye saa tano au saa kumi tunakula yogurt tena ile ya asas ambayo ni low fat na sio tamu haina sukari ni plain.
10.Kusnack pia unakula matunda kama vile aple,chungwa,matunda jamii ya zabibu,jamii ya baries na mapeasi.Matunda haya yamechaguliwa mwanzoni kwani yanasaidia sana kuboost metabolism ili chakula kuyeyushwe haraka tumboni.Pia yana kiwango kidogo cha sukari.
11..Alfajiri ukiamka unakunywa kikombe cha maji ya moto yenye limao.Yanasaisia kurahisisha mmeng'enyo aa chakula kwa siku hiyo.
12.Kila baada ya mlo utakuwa green tea haya ni majani ya chai yale ya kijani sio meusi.Inamaana kwa siku vikombe vitatu asubuhi,mchana na usiku.
13.Hakikisha unakunywa maji sio chini ya lita 2 kwa siku maji yanasaidia sana kupunguza weight na pia husikii njaaa ukiyanywa ipasavyo.
MANUNUZI
1.green tea
2.yogurt zile za asas plain ambazo hazina sukari na ni low fat.
3.Matunda machungwa,peasi,zabibu,grape fruit,barries zile za aina zote.
4.Mafuta ya kupikia ya olive oil
5.Mayai
6.Samaki
7.Kuku mimi hununua vile vidari ambavyo vishawekwa kwenye kipakti kimoja zinakaa 6.
8.Mboga za majani aina zooote unazozijua wewe.
9.Limao au ndimu