chaliko
Senior Member
- Apr 1, 2019
- 180
- 804
Ninawaslimu wote kwa Jina lipitalo majina yote.
Awali ya yote niseme tu kuwa
1. Taarifa yangu ipo katika mfumo wa Swali.
2. Sina lengo la kuchafua Taasisi au mtu yeyote katika taarifa hii.
3. Nitakacho andika hapa nimekifanyia uchunguzi binafsi.
Leo naomba niwasilishe uchunguzi mdogo niliofanya juu ya Dayosisi ya Central Tanganyika ambayo ipo chini ya KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA. Kabla ya kuwasilisha uchunguzi wangu naomba nielezee mambo machache.
ENEO
Dayosisi ya Central Tanganyika (DIOCESE OF CENTRAL TANGANYIKA known as D.C.T), hii ni moja ya Dayosisi kubwa ambayo inapatikna katika Mkoa wa Dodoma. Dayosisi hii ina vitengo mbalimbali ambavyo vinafanya kazi chini yake huku ikimiliki Taasisi kama vile Makanisa, Vyuo, Shule, Hosipitali n.k
Askofu: The Rt Revd Dickson Chilongani
Anuani: Mackay House, PO Box 15, Dodoma, Tanzania
Simu ya Ofisi: +255 (0)26 232 4518
Web-site: www.d-c-t.org
Katika uchunguzi wangu nimegundua yafuatayo;
MICHANGO YA LAZIMA
Dayosisi imekuwa ikiwachangisha kwa lazima Wafanyakazi wake wote katika vitengo mbalimbali michango kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kikanisa. Mfano Mwaka 2019 Dayosisi iliwalazimisha wakuu wa Vitengo kuwakata wafanyakazi kiasi cha Ths 100,000/= ili kuchangia jengo la Kitega Uchumi linalojengwa mbele ya Kanisa Kuu.
MISHAHARA NA STAHIKI
Dayosisi imekuwa haiwalipi Wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali vilivyo chini yake Mishahara na Stahiki zao kwa wakati. Wafanyakazi wengi wamekuwa wakifanya Kazi miezi hata zaidi ya Minne (4) bila kulipwa na hata wanapolipwa hulipwa kidogo kidogo. Mfano katika Shule moja waalimu hawajalipwa Mishahara kwa Miezi zaidi ya Mitano (5) sasa.
MICHANGO YA PENSHENI
Dayosisi ya Central Tanganyika imeshindwa kuvibana vitengo vyake kuwasilisha Michango ya Pensheni ya Wafanyakazi wake kwa muda mrefu licha ya Wafanyakazi hao kukatwa katika Mishahara yao. Katika kitengo kimojawapo cha Dayosisi Michango ya Wafanyakazi haijawasilishwa kwa zaidi ya Miaka Miwili (2) NSSF licha ya Wafanyakazi kukatwa. Jambo la kushangaza ni kwamba hata wao NSSF wamekuwa kimya katika kudai madeni yao.
MADENI KATIKA BENKI
Dayosisi imeingia katika Mgogoro mkubwa na Mabenki baada ya Wafanyakazi ambao walidhaminiwa na Dayosisi kukopa fedha katika Taasisi hizo kushindwa kulipa Madeni hayo ama kwa Makusudi au la. Migogoro ya aina hii imepelekea baadhi ya Benki kusitisha Mikataba na Dayosisi ya kukopesha Wafanyakazi wake. Mfano halisi ni Benki ya CRDB ambayo imesitisha kabisha Mkataba wake wa kuwakopesha Wafanyakazi wa Dayosisi.
KUSHINDWA KULIPA KODI
Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa Taasisi nyingi zilizo chini ya Dayosisi zimekuwa zikikwepa au hazilipi Kodi. Hata pale ambapo Watumishi wa TRA walipo baini ukwepji huo wa Kodi na kuziandikia Bili, Taasisi hizo zimeshindwa kulipa kodi husika. Kabla ya mfumo mpya kuanza Taasisi nyingi za Dayosisi zilikuwa zikiwakata Wafanyakazi kodi ya Mapato bila kuiwasilisha TRA pia zilikuwa hazilipi Kodi mbalimbali. Kwa ujumla Dayosisi inadaiwa Mamilioni ya Fedha kama kodi lakini ulipwaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na,
i. Kukosa fedha za kulipa.
ii. Kukingiwa kifua na Waziri mmoja aliyekuwa Madarakni Awamu ya Tano, ambaye pia ni Muumini wa Dayosisi hiyo.
Baada ya uchunguzi wangu huu binafsi nimejiuliza:
JE, DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA INAENDESHWA KIHUNI?
Ahsanteni.