Hii lugha ya: "angekuwepo wangemsema....."mnapenda sana kuisema sema. Magufuli alipokuwepo watu walimsema, lakini utaona walichofanya(rejea Lissu na wengine). Baada ya kuona kumbe ukimsema kwa kumkosoa unafanywa hivi, watu wakanyamaza, Sasa ameondoka wanasema kitu ambacho walikuwa hawafurahi nacho. Kwa mfano, Magufuli alivyowaambia Wakurugenzi mpinzani akishinda eneo lako wakati nakulipa vizuri, sijui utanieleza nini? Matokeo yake wapinzani wanaporudisha fomu, Wakurugenzi wanakimbia ofisi. Je, kwa uchaguzi wa aina hii, unategemea Taifa lipate viongozi wa aina gani? Watu Sasa wanasema akiwa hayupo.