Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Linapokuja suala la Afya ya viongozi hilo ni suala mujarabu kabisa kwa umma kuhoji.
Leo akiongea bungeni, Dkt. Mpango ameonyesha kwamba hata yeye alikuwa hana taarifa zozote za kuteuliwa kwake kuwa Makamu wa Rais, hii maana yake ni kwamba hili suala limefanyika kwa usiri mkubwa bila hata yeye kujua.
Tunajua ni majuzi tu Dkt. Mpango alikuwa hoi bin taaban kwa maradhi yanayohusishwa na ugonjwa wa Korona, Tulimuona akikohoa kwa nguvu huku akioneana mchovu sana.
Swali ambalo mimi kama raia ningependa kuuliza, Je Dkt. Mpango yuko physically fit kushika majukumu mazito ya kumsaidia Rais katika nafasi hii aliyopewa?
Tuliona mathalani, Hayati Magufuli alikuwa ni mgonjwa wa muda mrefu wa Ugonjwa wa Moyo, na kama mnavyojua kazi ya Urais ni kazi nzito yenye stress nyingi na bila shaka siyo rafiki kwa watu wenye ugonjwa wa moyo, Je Vetting process ililifikiria hilo suala kabla ya kumpa Magufuli green light ya kugombea urais?
Je, na mfumo wa vetting nchini umelifikiria suala la Dkt. Mpango kuwa makamu wa Rais, Je wamejiridhisha kuwa yuko fit kwelikweli baada ya kuugua Covid-19?
Kitu kingine ninachomshangaa Dkt. Mpango ni kuwa havai barakoa kwenye mikusanyiko, Je akipata Covid tena katika mazingira ya sasa, ukilinganisha na athari ambazo Covid ya kwanza iliupa mwili wake je atakuwa katika hali gani?
Ni wakati muafaka sasa afya za viongozi wetu ziwe ni factor mojawapo kwenye vetting, la sivyo hii ni disaster kwa nchi