Je, Dkt. Wilbroad Slaa anajipenyeza CHADEMA kiaina kuimaliza kazi aliyopewa na CCM?

Tatizo unakalili maisha hakuna mfanano wowote katika mageuzi yoyote duniani ccm itatoka tu madarakani tena sio sababu ya uimara wa chama chochote cha siasa itakuwa ni maamuzi ya wananchi hawa mnaokesha kuwakatia umeme kila siku na kukandamiza haki zao, ipo siku mtashangaa sana kobe kuinua kichwa na miguu ya mbele.
 
Hapana.

Mi najibu mada kufuatana na nilivyoelewa Kichwa cha mada yenyewe. Sijasoma hayo maandishi mengi chini yake.

Usichanganye mambo. CCM ya Magufuli, kamwe siyo CCM ya Samia. Hili tulishaliwekea mada yake yenyewe humu humu JF.

Kwa hiyo dhana ya kwamba Slaa anaendelea na kazi ile ile aliyotumwa kuifanya chini ya Magufuli, na sasa aiendeleze chini ya Samia, hiyo ni dhana batili, potofu kabisa.

Ni sawa na kusema kuwa, mapambano ya CHADEMA dhidi ya CCM ya Magufuli, ndiyo yale yale yanayoendelea chini ya Samia.
Wengi bado hawataki kuuelewa ukweli huu, lakini Mbowe aliyekuwa akipambana na Magufuli kwa gharama kubwa sana, siyo Mbowe yule yule anayepambana na Samia.
Hili nalo tulishalieleza vizuri tu humu humu JF.
 
Hakika "haina makosa." Muda si muda tuatona kazi yake ikitimia kuinusuru Tanzania, (tena)!
Siyo lazima mtu afe ndipo kazi isiyo makosa itimie.
Mbona kila siku inatimia. Au wewe unaijuwa saa yako ya kuondoka itakuwa lini?
 
Umeuliza swali nimekujibu, au ulikuwa hujuwi kinachojadiliwa?
Sasa unataka huu nao uwe mjadala pembeni ya mada husika?
Ukitaka kwenda hivyo tutakwenda tu, kama ujuavyo hapa hakuna lelemama.
 
Sasa unataka huu nao uwe mjadala pembeni ya mada husika?
Ukitaka kwenda hivyo tutakwenda tu, kama ujuavyo hapa hakuna lelemama.
Ukiuliza swali utajibiwa na kuulizwa kwa mujibu wa swali lako.

Wewe unaijuwa siku na saa yako ya kufa?
 
CHADEMA wakalipokea hilo. Wakasimama kiume, likapita na wakafanikiwa kuvuka salama...[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A
Analysis nzuri!
 
Dr Slaa alituumiza moyo sana Watanzania.
Siasa ni Itikadi sio ujasiliamali!

Unaweza kumlamu Dkt Slaa kama utakubali kuwa siasa ni ujasilimali ila ukiwa unaamini siasa ni itikadi huwezi mlaumu Slaa kwa alichofanya 2015.
 
Sauti ya Watanzania ni mpango mzima wa TISS ya CCM kama ndoano ya kuwanasa CHADEMA wajae wenyewe kisha wajimalize. Hongera Freeman Mbowe na chama chenu kwa kutumia macho yeu ya ndani kuuona mtego huo..!
Baada ya kukusoma sasa, bado nasimamia pale pale pa mwanzo.
Ukitaka kujua jinsi Samia anavyoiua CHADEMA, kazi iliyoshindikana wakati wa Magufuli, siku nyingine elekeza fikra zako kwenye mbinu mbadala anayoitumia Samia kuifanya kazi hiyo, bila ya kutumia mabavu ya Magufuli.

Mwenyekiti Mbowe alishanasika siku nyingi, sasa kazi ngumu anayoifanya ni kulainisha upinzani uliomo ndani ya chama chake, ili CHADEMA isalimishwe kwa CCM ya Samia.

Wimbo uliopo mashuhuri sasa hivi, na unaopanda kwa kasi 'chart' zote, ni kushirikishwa CHADEMA katika serikali ya Umoja.

Sina lolote la kumtetea William Slaa baada ya mengi uliyoeleza na zaidi; lakini ninachokubaliana naye kwa sasa ni kukataa hayo wanayoyakataa kuwa siyo maslahi ya nchi yetu.
Kama hawa watu ni sehemu ya upotoshaji unaotumiwa na CCM kupitia hiyo taasisi ya TISS, hilo silijui, na kama lipo, sijali iwapo hadaa hiyo inaeleweka kuwa nimapambano dhidi ya CCM katika kila sura yoyote inayojionyesha. Kuna siku hadaa hiyo itagota, na ndiyo utakuwa mwisho wa CCM.

Naona leo kumekuwepo na 'project' nyingi kumhusu huyu mtu mmoja Slaa; hivi kampeni ya pesa za waarabu tayari zipo kazini, au vipi?

Ni vigumu kuamini kuwa baadhi ya watu kama mleta mada naye anaweza kuingia kwenye mtego hafifu kama huo.
 
Erythrocyte please take note of this thread/post! Ameongea mambo ya msingi sana. Kaeni mbali na hili kundi la sauti ya watanzania! Wafanye program zao na Chadema ifye program zake ingawa zote zina lengo moja, KATIBA MPYA NA BANDARI/RASLIMALI ZETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ