Je, Dkt. Wilbroad Slaa anajipenyeza CHADEMA kiaina kuimaliza kazi aliyopewa na CCM?

Chadema wao peke yao hawawezi kuja kutokea waitoe ccm, NEVER !!

Inabidi kuwe na vyama ziada vya upinzani na kuwe na muungano wa hivi vyama sio mpaka kampeni zifike.
Vyama vipi hivyo vya upinzani unaviongelea?....hivi ambavyo mpaka sasa havijaweza kufanya hata mkutano mmoja wa kuvuna wanachama?
 
Hapana
 
Nilidhani utajifanya huelewi, kumbe unakiri jibu ndilo hilo.

Kazi ya Mungu haina makosa.
Unaanza 'ulevi', ambao sina simile nao.

Isingekuwa na makosa asingekuwepo shetani kama kweli yupo. Hao miungu wenu mnaowaamrisha nyinyi walevi levi mnaoendeshwa na huyo shetani anayeruhusiwa na mungu awaendeshe.

Ni hivi, unapotaka mjadala na mimi, ondoa 'ulevi', sina muda na takataka hizo.
 
Shtani ni fifa ambayo ipo kwa viumbe. Hakuna cha ajabu kabisa hapo, hata wewe ni shetani.
 
Ccm ni ileile mkuu! Subiri harakti za uchaguzi zianze hapo ndio utaona sarakasi za ccm.
Usinielewe vinginevyo.
Jina ni lile lile, CCM, lakini kama chama cha siasa, kila mwenyekiti anayeshika nafasi hiyo ndo anakuwa dereva wa dubwasha alilokabidhiwa, na analifanya vyovyote apendavyo yeye.
 
Mimi ni bint adam, sina sifa ya ushetani. Hiyo unayo wewe.
Ushetani unauonyesha kila siku katika fikra na mawazo yako.
Hata shetani kama yupo, naye hujitangaza kuwa ni malaika, sembuse wewe?
 
Kianzishwe chama na mtaji wakwanza ni wasafwa hawa jamaaa hawajawai ikubali ccm
 
Ushetani unauonyesha kila siku katika fikra na mawazo yako.
Hata shetani kama yupo, naye hujitangaza kuwa ni malaika, sembuse wewe?
Hakuna shetani mwenye uwezo wa kujitangaza kuwa ni malaika. Kufikiri hivyo ni ujinga.
 
Dr Slaa huwa hana aibu wala soni! Chadema wamekuwa wastaarabu kumstahi kupita kiasi!
1. "siwezi kuthibitisha kuwa mbowe siyo gaidi" Dr Slaa balozi wa Tz Sweden
2. " Ni kawaida ya watu kupigwa risasi na kuuawa kwa lissu siyo jambo geni wala la ajabu" Slaa Balozi Tz Sweden
3. "Chadema wana tabia ya kutekana kwa hiyo hata hili la Lissu ni mlolongo ule ule" Slaa Balozi Tz Sweden
4. " Ni lazima tuungane wote tupiganie haki ya Nchi yetu na raslimali zetu" Slaa raia wa Tz Balozi mstaafu
5. "Tutafanya maandamano nchi nzima ili kuikomboa nchi yetu na huyu mama atakimbia kiti" Slaa aliyenyang'anywa hadhi ya ubalozi.

Huyu Nyoka makengeza akimbilie mbali A nasty and dirty opportunist to have around
 
Kwani siasa ni uadui? Muda wa uadui ukifika hata msituni itaundwa wing ya "msituni", LAKINI LEO NGOJA TUIPE DIPLOMACY ITS STAKE IN THE FUTURE OF TANZANIA/TANGANYIKA
Unapochanganya maana ya "siasa" na "Maslahi" inakuwa vigumu kujua unaongelea jambo lipi kati ya hayo mawili.

Tanzania hakuna siasa, kuna utafutaji wa fursa na maslahi.
 
Nadhani kwa sasa alishatumika na CCM kama Toilet paper,hana jipya! Anachopaswa kufanya ni kukiomba radhi chama cha CHADEMA kwa kukichafua chama pamoja na kuuza sera za CHADEMA kwa CCM.
Lakini hata hivyo upande wa pili bado ana ushawishi mkubwa katika medani za Kisiasa! Si mtu wa kupuuza,bado ni Mzalendo mzuri wa nchi yetu.
Chadema fikirieni kumrudisha kama ataomba radhi.
 

CHADEMA INAVYOISAIDIA CCM KUSHINDA KWA ZAIDI YA 98% UCHAGUZI UJAO

Na Mwl Udadis, Tarime

Moja ya kosa kubwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanafanya na ndio inayopelekea wao kuendelea kushuka kila siku ni kudhani kuwa kupendwa na watu ni miujiza au kuna njia fulani ya mkato, ni mawazo haya yanawaaminisha kuwa ndani ya miezi 24 ijayo yatatokea maajabu fulani kisha wao watashinda Uchaguzi. Fikra hii haina tofauti na kuamini mazingaombwe.

Badala ya kufanya kazi hivi sasa Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wanagombana kwa madai kuwa Mbowe amechukizwa kitendo cha kundi la Dkt. Slaa na Wakili Mwabukusi kukusanya fedha kwaajili ya kuendesha mikutano bila kumshirikisha yeye na kisha kutaka kuwashirikisha Chadema katika hatua za mwisho. Msingi wa madai ya kundi la Mbowe yamejengwa katika tamaa ya fedha na ni uthibitisho wa namna baadhi ya viongozi wa Chadema wanavyotumia siasa kujinufaisha badala ya kujenga chama chao.

Wakati huo huo Ndugu Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama yeye bado yuko Ubeligiji akidai anajipumzisha kidogo baada ya kufanya mikutano katika Mikoa Mitatu. Japo habari za chinichini zinadai yuko katika matibabu kutokana na kuzorota kwa Afya ya akili bado wataalam wa siasa na mikakati wataungana na mimi kuwa Chadema imelala na inakisindikiza Chama cha Mapinduzi katika ushindi wa zaidi ya Asilimia 90.

Ni ukweli usiopingika kuwa ulozi au "Abracadabra" kwenye siasa haipo, hivyo Chadema inapaswa kufanya kazi kama CCM wanavyofanya yaani kufanya ziara, kutatua matatizo au kutoa njia mbadala, kusikiliza watu wanasema nini badala ya kujikusanya katika "WhatsApp group" na kutoka na maazimio ya kihuni ambayo wachangiaji wanayatoa wakiwa bar ya triple seven Mikocheni.
 
Slaa katumwa na Kinana hakuna asiejua.
 
Sababu za Mbowe kuachia njiani mjadala wa Bandari kuwa Wana mambo mengi au hawakushirikishwa mapena ni za kitoto.

Wangetwambia HOFU Yao kushirikiana na Mwabukusi & co ni ipi tujue mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…