Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa namna ya hili sakata la Hawa wanaojiita wabunge wa viti maalum, kupitia chama kilichowavua uanachama wao cha Chadema na namna Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, anavyojaribu kuendelea kuwakumbatia hao akina Halima Mdee, naziona dalili zote za kutokea kile kilichotokea kwenye ile Kesi ya kubambika ya ugaidi ya Mbowe na wenzake.
Nasema hivyo kwa kuwa Katika "proceedings" za Mahakama, kila kitu kitakuwa wazi.
Kwahiyo wale waliofoji barua na kupeleka NEC watajulikana.
Hata yule aliyemtoa mfungwa Nusrat Hanje usiku na kesho yake asubuhi akaenda kuapa na kuwa Mheshimiwa Mbunge,naye atajulikana wazi!
Huyo Spika Tulia Ackson, anayefanya sarakasi zote hizi za kuendelea kuwakumbatia wabunge ambao Hawana chama, lazima atambue jinsi anavyojitumbukiza kwenye shimo la kujiangamiza.
Tutarajie tena kushuhudia mashahidi wa akina Halima Mdee, toka NEC na Ofisi ya Bunge, wakiomba udhuru wa mara kwa mara kwenda "maliwatoni" kwenda jisaidia.
Je, DPP kwa mara nyingine tena, atalazimika kuiondoa mahakamani, Kesi hiyo kama ilivyomkuta aibu, baada ya kuiondoa Kesi ya kubambika ya ugaidi ya Mbowe na wenzake?
Yetu macho, tutege masikio yetu kwenye Mahakama Kuu, kushuhudia jinsi jopo la mawakili waliobobea la akina Kibatala, jinsi "linavyowagaragaza" mawakili wa akina Halima Mdee!😄