Je, DPP atalazimika kuiondoa Kesi ya akina Halima Mdee kama alivyofanya kwenye Kesi ya ugaidi ya Mbowe?

Je, DPP atalazimika kuiondoa Kesi ya akina Halima Mdee kama alivyofanya kwenye Kesi ya ugaidi ya Mbowe?

Kwa namna ya hili sakata la Hawa wanaojiita wabunge wa viti maalum, kupitia chama kilichowavua uanachama wao cha Chadema na namna Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, anavyojaribu kuendelea kuwakumbatia hao akina Halima Mdee, naziona dalili zote za kutokea kile kilichotokea kwenye ile Kesi ya kubambika ya ugaidi ya Mbowe na wenzake.

Nasema hivyo kwa kuwa Katika "proceedings" za Mahakama, kila kitu kitakuwa wazi.

Kwahiyo wale waliofoji barua na kupeleka NEC watajulikana.

Hata yule aliyemtoa mfungwa Nusrat Hanje usiku na kesho yake asubuhi akaenda kuapa na kuwa Mheshimiwa Mbunge,naye atajulikana wazi!

Huyo Spika Tulia Ackson, anayefanya sarakasi zote hizi za kuendelea kuwakumbatia wabunge ambao Hawana chama, lazima atambue jinsi anavyojitumbukiza kwenye shimo la kujiangamiza.

Tutarajie tena kushuhudia mashahidi wa akina Halima Mdee, toka NEC na Ofisi ya Bunge, wakiomba udhuru wa mara kwa mara kwenda "maliwatoni" kwenda jisaidia.

Je, DPP kwa mara nyingine tena, atalazimika kuiondoa mahakamani, Kesi hiyo kama ilivyomkuta aibu, baada ya kuiondoa Kesi ya kubambika ya ugaidi ya Mbowe na wenzake?

Yetu macho, tutege masikio yetu kwenye Mahakama Kuu, kushuhudia jinsi jopo la mawakili waliobobea la akina Kibatala, jinsi "linavyowagaragaza" mawakili wa akina Halima Mdee![emoji1]
Tujikumbushe kidogo! Hii ni kesi ya madai, sio JINAI! DPP haingizi mkono huko!
 
Samia Suluhu anataka ithibitike kuwa yale makesi yoote yeye hahusiki nayo. Ndio maana anayaacha yaendelee ili walioyatunga wawe wanaumbuka wenyewe.

Tuliona kesi ya Akina Mbowe mambo yalivyokuwa

..mbona ktk mahojiano na bbc Raisi aliunga mkono kesi, na alidai kuna washirika wa Mbowe walishahukumiwa?

..kwa mtazamo wangu, Ssh alijaribu kumfunga Mbowe, tatizo ni kwamba waliokabidhiwa jukumu lile walikuwa na uwezo mdogo ktk kutengeneza kesi ile.

..Ndio maana unaona Kingai kapandishwa cheo. Ujue kwamba ni amebeba siri nyingi za mipango miovu ya watawala.
 
Sasa kama chadema hawataki viti kule bungeni tujuze kilichowafanya kina hawo halima kupokonywa ubunge wao kwemye ucahguzi wa 2020 nini?

Kwanini magu alitumia nguvu kubwa ya kuweza kuua,kuweka kura feki n.k mabaya ili tu chadema wakose ubunge akiwemo huyo halima.


Sasa wao wamepelekwa ni serikali ila wanatumia chama chá chadema Kwanini wasitumie ccm kwa vile wameshafukuzwa?

Waliishitaki chadema Sasa bila ya chadema kuenda mahakamani itakuwaje?


Hili ni tatizo lenu nyinyi ccm mlilolifanya 2020 kwa ujinga wenu.


Chadema wanaubavu wakumtoa mfungwa ili akaapishwe na awe Mbunge?

..ubunge wa kina halima ni matokeo ya ujinga wa Ccm ya Magufuli.

..Ccm za awamu zilizopita walikuwa hawaibi kwa pupa na ujinga kama wa 2020.

..awamu zilizopita walikuwa wanaiba huku wakiruhusu idadi fulani ya wapinzani waingie bungeni ili kuficha aibu kuwa Ccm wameiba uchaguzi.
 
Wenye akili timamu tumekuelewa japo wewe ni Mwana kijani ila kwenye ili umesema Ukweli Mtupu ndio maana msimamo wangu kuhusu Afrika ni kwamba Bwana Trump alikuwa sahihi juu yetu watu weusi...

..Kuna forgery.

..Kamati Kuu ya Cdm haikuteua viti maalum.

..Na wagombea au wabunge wa chama chochote huteuliwa na vikao si vinginevyo.

..Yeyote yule ambaye amepata uteuzi bila kuhusisha vikao halali vya chama atakuwa amegushi, amedanganya, au ametapeli.

NB:

..hata kama kuna saini ya Mwenyekiti, bado watakwama kwa kuwa Kamati Kuu haikuteua.
 
Back
Top Bottom