Je, DPP atalazimika kuiondoa Kesi ya akina Halima Mdee kama alivyofanya kwenye Kesi ya ugaidi ya Mbowe?

We nae hamna kitu. Sasa wangesaini harafu wakawafukuza,
 
Mkuu, sasa kesi ya kina Halima inamuhusu vipi DPP. Siyo kila kesi iliyo mahakamani ni ya DPP.
Msamehe bure,labda anazani DPP ana mamlaka ya kukamata,kupeleleza na kupeleka kesi Mahakamani,na kuondoa kesi Mahakamani vile vile!!!!
 

Chadema mnakosa hoja Sana,

Nyie hamtaki vile viti, na mlisema public,

Sasa mna makelele ya nn? Akili yenu tumeijua wale ni wabunge mpaka 2025

Huko mahakamani mnagaragzwa mpaka mtashangaaa
 
Kama kuna utata wa Sahihi kugushiwa,si wapeleke malalamiko yao kwa Wataalamu wa Uchunguzi wa kisayansi juu ya hati na Sahihi pale forensic!! Jinai inataka Victim ndiyo uisibitishe kwanza kwa taarifa!!
 
Yetu macho, tutege masikio yetu kwenye Mahakama Kuu, kushuhudia jinsi jopo la mawakili waliobobea la akina Kibatala, jinsi "linavyowagaragaza" mawakili wa akina Halima Mdee!😄
Sijui kama hii kesi itafika kote huko!, sisi wazee wa masauti tumeisha sikia Sauti na tumeileta humu The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia!

Ila pia powers za DPP ni kwenye kesi za jinai, kwenye kesi za madai, au kesi nyingine zote DPP hana mamlaka hayo.

Kiukweli kuna uhitaji mkubwa wa elimu basics ya sheria kwa wananchi kuelimishwa the basics za sheria, mahakama, Bunge, serikali na haki zao.

P
 
Maghakama ghuru eti???
 
CCM na Mkt wao majuzi si wameazimia kuziondoa kesi zote za kisiasa mahakamani. Pili kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa? Tunapata je imani toka wananchi kwa yale tunayoyasema..

 
Hivi toka lini DPP akahusika na kesi za madai?
 
Fahamu kwamba ,Kuna taasisi za serikali zinahusika kwenye madai husika,mfano tume ya taifa ya uchaguzi.
Kwa hiyo kila kesi ya madai iliyopo mahakamani Ina hao mawakili wa taasisi za serikali? Mbona haya ni mapya tena?

Tuache kipenga kilie mpira uanze. Ila serikali itaumbuka na hasa time ya uchaguzi na Spika wa Bunge.
 
Yule Tumbili -Tulia angeitwa kutoa ushahidi mwenyewe ingekuwa poa sana yaani lakini baasi tena walisaidiana kuvaa gamba majuzi tu>. Lakini serikali inaenda kuumbuka tena kwa kishindo cha ajabu. Mipango ya kuwadai hao waasi mabilioni ya kodi wanazolipwa bila kustahili iko mbioni. Diwani atamuoa halima mke wa tatu!
 
Umeshawahi iona hiyo barua unayosema imesaini na kuwekwa muhuri?
Na Kwa nini hujiulizi mbona NEC hawajaiweka hadharani hiyo barua?
Ukweli unajulikana hakuna barua yeyote kutoka chadema kwenda NEC kuwateua hao covid.
 
Basi Chadema kiboko, kwa hiyo walikwenda mpaka singida wakamtoa Nusrat jela usiku na kumleta bungeni kula kiapo? Yaani kifupi wewe ni mjinga. Kama hili nalo umeshindwa kuelewa, majibu ya Ndugai unayakumbuka wewe? Kwamba kwa akili ya Ndugai awe anajua Chadema walihusika lazima angeitisha press na kuwaonyesha ushahidi alionao tena nyuma yake yupo Magu. Nini kinazuia kuonyesha hizo nyaraka ili kuwaibisha Chadema!! Wamejaribu kesi ya kishamba ya kumbambikia ugaidi mwenyekiti Mbowe wamekwama sembuse wawe na hizo nyaraka!!
 
Tafuta chakula cha watoto wako!
usihangaike na haya mambo hutayaweza ni ushauri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…