Je F.Mbowe anafaa kuwa RAIS?

Hayo mabilioni yanayochukuliwa mbele za macho ya jk na kuendelea kuwateua wengine ambao bado wana kashfa za ufisadi kwenye baraza la mawaziri ndio sifa a kuendelea kuwa raisi?

Mabilioni yalichukuliwa wakati wa borther ben, lakini nayo yako jikoni, "tunayashughulikia" na hayo usemayo yanayochukuliwa wakati wa JK , nadhani wewe mwenyewe ni shahidi wa action zilizopo. Uchunguzi wa BoT ulifanywa na serikali anayoongoza nani? Na kamati ya hilo saga infanywa na serikali inayoongozwa na nani, kamati ya Mwakyembe..., Kamati ya Buzwagi... "Action speaks louder than words".
 

Field Marshall ES,

Heshima mbele zumbe,
Nilimsikiliza Mh. Philipo Marmo, Waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Mambo ya Bunge) Wakati anachangia mjadala wa Richmond..

Alisema Hii ni kamati ya nne au ya tano tangu Tanganyika huru... na kamati hizo zote za Bunge zilileta impact kubwa katika nchi yetu! Nadhani utakubaliana nami kwamba kuna nyingi za hizo kamati ziliundwa wakati wa Chama Kimoja.

Na nadhani utakubaliana nami kwamba Bunge letu kwenye muongo mmoja hivi (miaka takribani 10 iliyopita) lilirudi nyuma kwa sababu tu ya ushamba wa demokrasia ya vyama vingi bungeni! Wabunge wakasahau kuwakilisha wananchi wakawa wanawakilisha vyama vyao... ndio maana kuna wakati wananchi walilalamika kwamba bunge la chama kimoja lilikuwa vibrant hata zaidi ya la vyama vingi... hata hivyo nadhani tulikosea, tumejifunza na sasa watu wanarudi.

(Nikumbushe tu kwamba kwenye serikali ya Mwinyi wabunge hawa waliingia kwenye serikali kwa sababu ya kuichachafya serikali na sio kwa kuwa walikuwa viongozi wazuri.. Mg. Augustion Lyatonga Mrama (Mambo ya Kawaha), Mh. Philipo Marmo, Mh. Fredrick T. Sumaye, Mh. Mateo Quares, Mh. Njelu Kasaka etc..) Jamaa walikuwa mwiba kwa serikali ya Mwinyi, Na Rais wetu mstaafu Mwinyi naye kawaida yake ilikuwa ukileta chokochoko unapatiwa Uwaziri au unaibu...

Kwa mstakabali huo ingekuwa Mh. Mwinyi ndiye angekuwa madarakani, sasa hivi... dada yetu Mh. Anne K. Malechela , Mh. Mwakyembe, Mh. Lucas Seleli, Mh. Shibuda, Mh. Eng. Stella Manyanya etc... wangekuwa mawaziri au manaibu mawaziri...

Mwisho niseme ni wabunge wa CCM ndio waliosababisha Mh. Lowassa (MB) Awajibike... lau ingekuwa tofauti... basi wangewajibika wangekuwa Mh. Msabaha na Karamaji tu!!!

Kwa hivyo basi lazima tukubali umuhimu wa Upinzani bungeni na mimi nimeendelea kuamini kwamba kutakapokuwa na uwakilishi wa 6.5 kwa 3.5; au 6.0. kwa 4.0; au 5.5 to 4.5 then hapo tutakuwa na nchi ambayo utani hautakuwepo tena... hapa mimi sijali chama kitachokuwa madarakani... nijuavyo chama hicho kitakachokuwa madarakani/tawala kitakuwa kinasimamiwa kweli na Bunge kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inavyotaka.
 

IF YOU HAVE NOTHING TO WRITE, DO NOT WRITE HERE.

UNAWEZA KUTUPATIA GHARAMA ALIZOTUMIA NI KIASI GANI KATIKA UCHAGUZI NA KUTUPA FIGURE HALISI ILIYOTOKA KATIKA 'BIASHARA' ZAKE?
 

MKUU FMES,
PAMOJA NA MAELEZO YAKO MAZURI, PLEASE JIBU SWALI KAMA MBOWE ANAFAA AU HAFAI.
 
Mkuu Pundamilia07,

Katika academic world, tunaposema kiongozi mmoja hafai, huwa ni lazima tuwataje wanaofaaa na sababu, kwa hiyo in this case nilitegemea ueleze jinsi Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, wanavyoafaa kuliko Freeman, meaning skills walizonazo ambazo ziliwafanya watufanyie taifa letu mambo mazito na mazuri sana, ambayo Freeman hawezi,

Mwalimu, hawezi kuingizwa hapo maana he is too much.

Ahsante Mkuu.
 
MKUU FMES,
PAMOJA NA MAELEZO YAKO MAZURI, PLEASE JIBU SWALI KAMA MBOWE ANAFAA AU HAFAI.

Siku zote nilikuwa nadhani, Mbowe ni mtu mwenye uelewa mkubwa sana!!! Kwa mshangao mkubwa, walipokuwa wanahojiwa TVT mbowe, Warioba, Butiku, Hamad rashid na Mama malechela. Wakati Butiku anaeleza utaratibu wa Rais kuteua mawaziri, anaweza kushirikiana na Waziri mkuu, Mbowe akaingilia na MAKAMU WA RAISI!!!! wale wazee wakamwambia! Hapana kijana, VP hahusiki!!! Nahisi, Mbowe aliona aibu!!!

Kabla ya hapo, ningesema mbowe anafaa kuwa rais, ila kwa sasa itabidi nijiulize mara mbili. Pengine anaweza shughuli za urahisi tu bali si uraisi!!!!!


Mwafrika wa kike, hebu tusaidie, mteule anatuangusha!!!!
 
Mbowe nafikiri anaweza..ameweza kuwaletea wananchi maendeleo kabla hata hajawa kiongozi.Kama sio yeye upinzani ungekuwa umekufa hivi sasa!Ni mtu anaependa ushirikiano na asiye na madharau!Ana vision...ambayo itaisaidia kama akipata ushirikiano!Tatizo tulilonalo ni siasa za kibaguzi ambazo CCM inazikumbatia!Siasa za kuwatisha wananchi..eti vile ni mchagga!Ki hivyo hatuwezi fika..ni watanzania wenyewe tutakaoiletea nchi yetu maendeleo na si vinginevyo!
Mfano halisi ni huko Kenya..nilikuwa nikienda huko na nina familiy!Mtu akiwa mkikuyu hata awe masikini kiasi gani hawezi kuwa na imani na mjaluo..ama mkaleinjin..hata awe na sera nzuri kiasi gani!Ni sumu ya ubaguzi wa kikabila..kwamba tabaka flani linafaa na lingine no!stereotype ambayo mwishowe itatuangamiza wenyewe!Tukumbatie siasa za maendeleo!Kule Kenya chuki kama hizo zilianzishwa zamani na KANU kama CCM inavyoendelea kufanya!Kuna sehemu nyingine ukienda ukasema wewe ni mchagaa unawatia watu kichefuchefu!Hawataki hata kukusikia..let alone kukuona!Viongozi wote wakuu wa nchi walionyesha wazi chuki..Mkapa na Kikwete wamekuwa wakiwaleta viongozi wanaowachukia wachagga mkoani Kilimanjaro!Wengine wameonekana kuwa ni magaidi wenye roho kutu!Kama vile ZOMBE..ambaye baadaye alipoamishiwa Dar alifanya mauaji!Viongozi walifikiri ni mtu mfuatiliaji kumbe yeye mwenyewe ni gaidi na jambazi lenye uwezo wa kukutoa roho saa nusu!Ni wakati wa kukumbatia siasa za umoja na maendeleo!
 

..hivi,majuzi mzee wetu shein hakuhusika?
 

Duh hii noma mkuu...
 
MKUU FMES,
PAMOJA NA MAELEZO YAKO MAZURI, PLEASE JIBU SWALI KAMA MBOWE ANAFAA AU HAFAI.

Anafaa kuliko Kikwete mwenye ukiwete wa uongozi na Mkapa aliyetoka kapa. Kama uchaguzi wa 2005 ungerudiwa tena hivi sasa, ungemchagua nani kati ya Kikwete na Mbowe?

Asha
 

Mzee gani alisema hayo? Kama ni Butiku basi hajui anachokisema. Warioba ni waziri Mkuu, anajua kabisa kuwa Makamu wa Rais ni sehemu ya Taasisi ya Rais hivyo anahusishwa katika hili. Mbona Kikwete katika hotuba yake kwa wazee wa CCM wa DSM alisema wazi kwamba alimwita Shein Dodoma kwa mambo kama hayo? Hebu acha umbea wewe.

Kikwete ndiye aliyedhani Urais ni kitu rahisi, ndio maana bado anaendeleza sherehe. Akimaliza kumlete Bush atawaleta wakina Shakira na Madonna.

Haijaandikwa kwenye katiba kwamba VP anamshauri Rais kuhusu baraza, imeandikwa PM lakini kwa kuwa VP ni sehemu ya Urais- ndio maana ya kuwa mgombea mwenza. Anakuwa consulted.

Asha
 

Kazi kweli-kweli,
Sawa nimeshasoma maelezo yako, Je, Mbowe anafaa au hafai kuwa rais?
 
ss wakubwa kama jamaa atatumia kigezo hicho cha tvt kuwa mbowe hawezi kuwa raisi?je kikwete aliyepewa cheque ambayo ina maandishi yanayokinzana,je yy anaweza kuwa raisi?raisi asiye makini na anayoyafanya?inaonyesha hata anaposini misaada au mambo mengine huwa apitii kwanza anachokisaini kwa hiyo ni raisi kabisa kwa yy kusaini mikataba ya kutuuza cc na nchi yetu pasipo yy kujua.
 

Sawa kabisa Kwayu
 

Hao wachaga wameikosea nini nchi yao? kwa nini wachukiwe hivyo?

Maana katika uongozi wa nchi wameishia level ya uwaziri, hakuna PM wala Prezidaa.

Nauliza kwa nini hatuwapendi??
 
Hao wachaga wameikosea nini nchi yao? kwa nini wachukiwe hivyo?

Maana katika uongozi wa nchi wameishia level ya uwaziri, hakuna PM wala Prezidaa.

Nauliza kwa nini hatuwapendi??

..huo mtazamo [wa jmushi] uko twisted kidogo!amekuza mambo!
 
Mi naomba niseme badala ya kaunza smear campaign inayoendeshwa na Karl Rove wa CCM, hebu turudi kwenye mada yetu ya kuwa Mbowe anafaa kuwa rais au la. Mi nadhani tuanze kwa kuangalia vigezo muhimu ya kuwa rais wa URTz:
- Visionary: mtu anayeona mbali na ambaye ana mawazo madhubuti kwamba nchi iwe wapi baada ya miaka 5 na miaka 10
- Uniter: aweze kufanya kazi na vyama mbalimbali na pia aweze kuwasiliana na wananchi kwa njia mablimbali
- Mwadilifu: hii ni zaidi ya kuwa hana scandal. Ni uadilifu wa kazi na uadilifu katika maisha yake ya kila siku.
- Intelligent: tunahitaji mtu ambaye ana uwezo wa kifikra na anaweza kutathmini hali ya nchi na kuleta suluhisho. Hii haihusiani na kiwango cha elimu.
- Mchapakazi: hii si ile ya kusema eti anawahi kazini, bali awe mtu 'who can have things done', hata kama atafanya from 10 to 5pm au from 8 to 2pm hiyo haijalishi bali aweze kufanya kazi na asiwe mtu wa kutafuta easy solutions na cheap popularity.

Labda wenzangu mnaweza kuongeza vigezo vngine
 

..naongezea!

..anayeweza kuchagua timu bora ya kufanya nae kazi!
 

Hii habari ya brazameni naona wanaomtetea Mbowe wanashindwa kuijibu. Kwa nini? au hawaamini kuwa inawezekana kuwa hii gari ni ya wizi kweli? na inawezekana pia kuwa ushuru haijalipiwa au imelipiwa ki-mizengwe?

Tunaomba watu wa Interpol na TRA mnaopitia humu mumsafishe jina kiongozi wetu huyu wa CHADEMA au tunaomba Mbowe mwenyewe uliweke wazi hili, kwani nasikiya wewe mwenyewe ni mwana JF mzuri. Mimi nawapelekea hii post Interpol na TRA kwenye tovuti zao, kama watajibu haya kama hawajibu haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…