Je F.Mbowe anafaa kuwa RAIS?

Je F.Mbowe anafaa kuwa RAIS?

Kwa swala la ukabila sidhani kama chadema ni chama cha kikabila na kifamilia.Kwani viongozi wakuu siyo wachaga wote mfano, makamu mwenyekiti sio mchaga ,katibu mkuu sio mchaga,naibu katibu mkuu vilevile sio mchaga mwanasheria mkuu sio mchaga,mbunge wa tarime siyo mchga.ss huo ukabila uko wapi?CCM ndio chama cha kifamilia,cha akina karume,mwinyi,kawawa,na kikwete.vile vile ni chama cha kijeshi kwani viongozi wake wakubwa ni ma captain wote.kwanini CHADEMA iliyoweza kufichua ufisadi kiandamwe?jamani tuwe critical thinkers.
 
Hii habari ya brazameni naona wanaomtetea Mbowe wanashindwa kuijibu. Kwa nini? au hawaamini kuwa inawezekana kuwa hii gari ni ya wizi kweli? na inawezekana pia kuwa ushuru haijalipiwa au imelipiwa ki-mizengwe?

Tunaomba watu wa Interpol na TRA mnaopitia humu mumsafishe jina kiongozi wetu huyu wa CHADEMA au tunaomba Mbowe mwenyewe uliweke wazi hili, kwani nasikiya wewe mwenyewe ni mwana JF mzuri. Mimi nawapelekea hii post Interpol na TRA kwenye tovuti zao, kama watajibu haya kama hawajibu haya.

NO RESEARCH NO RIGHT TO TALK.naomba ututhibitishie kuwa hilo gari lake ni la wizi.
 
Nilikuwa namtangaza kwebye Star TV,Sijaona kama anaupeo mkubwa wa kuongoza nchini kwa jinsi alivyokuwa akilichambua Baraza la Mawazir.Mrema could a better Rais zaidi ya F.Mbowe.

wewe unawemaje?

Hafai kuwa Rais huyu.
Hana exposure wala elimu ya kutosha kuongoza vichwa vya Kitanzania. Ni mtu anayeigiza vizuri sana kwamba ana uchungu na nchi yake lakini kwa dhati kabisa amekaa kibiashara zaidi kuliko kujitoa kutumikia Taifa.

Angalau kijana wake Zitto anaonekana ni mtu mwenye uelewa na ufahamu wa mambo, nadhani hata kauenyekiti angemwachia jamaa.

Labda tumpe udiwani
 
NO RESEARCH NO RIGHT TO TALK.naomba ututhibitishie kuwa hilo gari lake ni la wizi.

samahani mkuu, si mimi niliyosema hayo, mimi nime-quote post ya brazameni naomba hili swali msukumie yeye.
 
Brazameni ile habari ya gari ya mbowe naona naulizwa mimi ushahidi wa hilo. Sasa sijuwi unawaambia nini kwa hilo?
 
..huo mtazamo [wa jmushi] uko twisted kidogo!amekuza mambo!
Upo twisted na nimekuza mambo kivipi?I have been through that kinda shit man!Sijui kuhusu Mbowe..lakini nadhani ameshakutana na hilo!NI WAZI...NIMESHAPATA SHIDA SANA KWASABABU TU YA UCHAGGA!Na hiyo inpain kwasana..NAPINGA UBAGUZI KWA NGUVU ZANGU ZOTE!GAIDI ZOMBE ALIKUWA MBAGUZI!MAHITA MWENYEWE..NI BAADA YA KUKAA KILIMANJARO KIDOGO NA KUGUNDUA KUWA NI STEREOTYPE TU ZA UKANDAMIZAJI LAKINI CHAGGA PEOPLE NI WAKARIMU KAMA WATANZANIA WENGINE!Ila aliletwa makusudi kwakuwa ni anti-chagga.NARUDIA TENA..MAENDELEO YA TANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA WENYEWE KAMA TUKIONDOA TOFAUTI ZETU NA KUJENGA TAIFA IMARA LENYE NGUVU!Kuacha siasa za uswahili na kuanza siasa za vitendo!Kuwapima viongozi kama wamewafanyia nini wananchi kabla hawajapata uongozi na si kusubiri wapate uongozi then kutueleza kuwa watatufanyia nini!Mbowe amewaletea wananchi maendeleo popote pale alipoweza..ubunifu na uzalendo..na kufanya kazi bila kujali utapata nini!A TRUE NON STARVING POLITICIAN..WHO WAS BORN A POLITICIAN!OTHERWISE ANGEWEZA KUENDELEA KUPONDA MALI TU..KWANI UNAFIKIRI ANATAKA UONGOZI KWASABABU UA NJAA?Other people talking about SUV?
 
Kwa kusoma posti zilizopo hapa inaonekana Mbowe hafai kwa kutumia vigezo vya Azimio la Arusha lakini sio haki zake za kiraia.
 
Hafai kuwa Rais huyu.
Hana exposure wala elimu ya kutosha kuongoza vichwa vya Kitanzania. Ni mtu anayeigiza vizuri sana kwamba ana uchungu na nchi yake lakini kwa dhati kabisa amekaa kibiashara zaidi kuliko kujitoa kutumikia Taifa.

Angalau kijana wake Zitto anaonekana ni mtu mwenye uelewa na ufahamu wa mambo, nadhani hata kauenyekiti angemwachia jamaa.

Labda tumpe udiwani

Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana . Unasema Mbowe hana Elimu ya kuongoza watanzania ? Hivi JK ana Elimu gani ya kutuongoza ? Kuongoza kwenye ndiyo huku ? Ukisema hafai ulete sababu . Azio la Arusha naona kuna mtu anasema hapa Mbowe halimshusu .Mbowe kakuta kuna mali na anaendeleza biashara za familia .Tena ni mtiifu jamaa hana hata kasoro moja ya kodi .

Unakumbuka kwa nini JK alikataa kwenda debate na Mbowe mwaka 2005 ? Hata leo wakiita debate kati ya JK na Mbowe utaona issue inavyo kuwa ya moto.Acheni chuki .Mbowe sasa anamaliza MSc yake ama hujui ? Ama kwako Elimu ni ya kwenda kuweka sahihi mikataba ya wizi na kuleta mvua toka Thailand ?
 
Bin Maryam:

Mawazo mazruri lakini hivi kweli ... "AZIMIO LA ARUSHA"..., Is this thing still valid? To the extent ya kumfanya Mtazania yeyote akose sifa ya kugombea uongozi?
 
Bin Maryam:

Mawazo mazruri lakini hivi kweli ... "AZIMIO LA ARUSHA"..., Is this thing still valid? To the extent ya kumfanya Mtazania yeyote akose sifa ya kugombea uongozi?

Yeye huyu binti kauliza na yeye maana hana uhakika .Ila wana maguo ya kijani na vikofia vya njano ndiyo wenye shida ya kupondea bila kusema kwa nini .Eti Elimu hawa ni wapuuzi sana . Mbunge wenu mmoja ka forge vyeti na polisi wanajua lakini kesi kashinda kisa JK kasema makelele ya mpangangaji nyote mnajua .Leo mnasema Elimu ikfika kwa Mbowe ama siyo ? PhD feki ngapi ziko kwenye Serikali ya JK sasa na ni mawaziri na manaibu ndiyo Elimu hiyo ?

Wizi wa gari nadhani ni maneno ya kijinga na fitina .Mbowe sawa na mpinzani mwingine kila siku wanatafutwa na sababu kibao hata ambazo ni personal life . Leo awe na gari la wizi toka UK wewe ujue na CCM wasijue wakaanza maneno yao na madongo anayo wamwagia ?

Akisha wabana utasikia wanakuja wanasema Chama cha kishikaji ama familia .Lakini tukianza kuichambua Chadema kuona famila ni ipi unakuta kimya .
 
Bin Maryam:

Mawazo mazruri lakini hivi kweli ... "AZIMIO LA ARUSHA"..., Is this thing still valid? To the extent ya kumfanya Mtazania yeyote akose sifa ya kugombea uongozi?

Azimio Jipya:

"you have to go to war with the Army you have, not the Army you want" Donald Rumsfeld's Doctrine.

Siasa ni kushiriki. Kama hatushiriki kwenye siasa itakuwa ni vigumu kuwapata tuwapendao.

Watanzania tunazo-criteria tayari za nani awe rais. Lakin hao malaika tuwatakao hawapo katika safu za siasa. Hivyo mtu achaguliwe kwa sababu angalau anaweza kufanyia kazi kitu fulani. Na wakati mwingine mtu mpya achaguliwe hili kuwapa mafunzo waliomtangulia.

Kwa mfano 1995 Mrema angechaguliwa sio kwa sababu atafanya kazi vizuri kuliko CCM, bali kuwapa shule CCM kwamba wasipofanya vizuri tutampa nafasi mwingine.

Mbowe anafaa kuwa rais hata kama elimu yake ni ya mwembeni
 
Naam Bin Maryam
 
wanasema eti baba yake aliuliwa na Nyerere
m36.jpg

Hii picha ina uhusiano gani na thread hii?
Nieleweshwe
 
Hao wachaga wameikosea nini nchi yao? kwa nini wachukiwe hivyo?

Maana katika uongozi wa nchi wameishia level ya uwaziri, hakuna PM wala Prezidaa.

Nauliza kwa nini hatuwapendi??
Walijaribu kiaina..umesahau mzee mwinyi alipofanya mambo nje ya katiba na kuanzisha cheo cha naibu waziri mkuu ili kumpa Mrema cheo ambacho hakikuwa kinatambuliwa kikatiba!Ile ilikuwa feki tu..Mrema mwenyewe anaelewa hilo!CCM wanasema CHADEMA ni chama cha kichagga?hio si ndo stereotype yenyewe ya kuwapotosha wananchi?
Na hilo swali la kuchukiwa siwezi kukujibu moja kwa moja..ila sipendi watu wanaochukia maendeleo..wananchi wana vipaji vya tofauti!wote kwa pamoja tutaijenga nchi yetu if we come together "solid"kwa nia nzuri ya maendeleo ya nchi yetu!Its the same thing with Obama in the US!Wamarekani wako mtegoni..he is the right guy at the right time for their country..lakini tatizo ni black na jina la kiislam!Wamarekani wanaonekana kuelekea kufungua ukurasa mpya wa siasa zao na kumchagua kiongozi based on the character!Same thing with our country!Hata kama Mbowe ni mchagga haina maana hataweza kuiletea maendeleo nchi yetu!He's got a positive mind....and his positive mind can turn to positive ideas..and if turned to positive ideas then we will be successfull!BUSINESS MENTALITY WHEN APPLIED HERE IS WHEN YOU DONT WANT TO SEE YOUR ACCOUNT IN NEGATIVE SIGN!YOU ALWAYS WANT IT TO BE POSITIVE..THE LATTER TOGETHER WITH PATRIOTISM THEN IT IS VERY CLEAR THAT WE WILL SEE THE LIGHT AT THE END OF THE TUNNEL!Kwamba ili kujenga taifa imara na lenye nguvu..ni lazima tuwe na viongozi wenye vipaji vya tofauti watakaotumia vipaji vyao together na uzalendo..na kujali watu..kuwahimiza kwenye shughuli za kimaendeleo,kuwapa elimu ya kutosha,kuwasaidia kwenye kilimo!Hayo ni mambo ambayo kiongozi kama Mbowe anaweza kuwafanyia watanzania!ONLY TUKIONDOA HIZO CHUKI NA KUWA TAIFA MOJA LENYE UHURU WA KWELI NA DEMOKRASIA YA KWELI!
 
Mkuu Pundamilia07,

Katika academic world, tunaposema kiongozi mmoja hafai, huwa ni lazima tuwataje wanaofaaa na sababu, kwa hiyo in this case nilitegemea ueleze jinsi Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, wanavyoafaa kuliko Freeman, meaning skills walizonazo ambazo ziliwafanya watufanyie taifa letu mambo mazito na mazuri sana, ambayo Freeman hawezi,

Mwalimu, hawezi kuingizwa hapo maana he is too much.

Ahsante Mkuu.

Pangekuwepo na uungwana JF, jibu hili lingefunga mjadala huu.
 
Kuna kitu sikielewi.

Ni kweli kuwa Mbowe gari lake ni la uwizi? Je huyo aliyetajwa ni kweli alilipwa hizo hela kupeleka gari Holland?

Mnaosema Mbowe ana faa. Anafaa kwa vigezo vipi?
Mnaosema hafai, mmetoa personal life yake kama hiyo ya gari n.k. Ila sijaona point yoyote ya MAANA mnayotumia kusema hafai.

By the way WHY NOW?. Hakuna uchaguzi kwa sasa. Tunzeni mawe yenu yaje kutusaidia 2010.

CCM Hoyeeeeeeeee!
 
Nawakumbusha uchaguzi wa 1985 na 1990, ambako kura ilikuwa Ndiyo kwa Mh. A. H. Mwinyi au Hapana (ndiyo kwa)Kivuli...
 
Back
Top Bottom