Je, Freeman Mbowe atajizolea pointi tatu muhimu kwenye press ya kesho?

Je, Freeman Mbowe atajizolea pointi tatu muhimu kwenye press ya kesho?

Anayetaka tumpe kula 2025. Akubali na alitaje kwa mazuri na wema. Jina lilo barika la kipenz wa watz. Dr. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI. maana walio taja vibaya 2020 Hatukuwarudisha bungeni.
 
Kipindi cha 2015-2020 ni kipindi ambacho wapinzani wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwa kukosa kuwa na uelewa wa wapi nchi inaelekea na wananchi wanataka nini hivyo ikasababisha anguko lao katika uchaguzi uliopita. Upinzani ukawa umepoteza uelekeo na kuaminika kwa watanzania.

Upande walioamua kuuchagua watanzania wa kuchagua wabunge karibu wote wa CCM ni upande sahihi kwa sababu watanzania waliona juhudi za JPM ni za kweli na halisi.

Kurudisha imani hiyo kwa watanzania inahitaji mikakati mikubwa zaidi ya waliyonayo sasa kwa sababu watanzania wataendelea kuuenzi uongozi wa JPM kama kielelezo cha mapambano ya kweli dhidi ya unyonge, kujiamini na kujitambua. Imani hii itadumu kwa muda mrefu mpaka kizazi kilichoshuhudia uongozi wa JPM wakiwa na akili timamu kitakapopotea na kufutika na hapo tunazungumzia si chini ya miaka 60 ijayo.

Magufuli ni ' living legend' ataishi ndani yetu miaka mingi sana.
CAG kamaliza kila kitu,,ataishi ndani yako wewe.
 
Upinzani ukawa umepoteza uelekeo na kuaminika kwa watanzania.
Huu uongo kama ule ibilisi.Imeandikwa,''Yeye asemaye uongo ni wa ibilisi manake yeye husema uongo toka mwanzo''Yohana 8:44.Wote tumeshuhudia uporaji wa kura wa waziwazi mchana kweupe.CCM ndiyo iliyopotea mpaka kutumia idara zote za serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kupora ushindi kwenye uchaguzi uliopita.Mungu ambavyo hadhihakiwi,jizi namba moja limeelekea jongomeo!
 
Zipo hoja nyingi zinazohitaji msukumo wa kisiasa, msukumo huo ni vigumu kuupata ndani ya chama Tawala ila utaupata upinzani.

Upinzani vyama vyote vimepoteza dira isipokuwa baadhi ya viongozi wa Chadema wanaweza kuendelea kuaminiwa kwa uvumilivu wao Hadi kuvuka salama mtihani wa uchaguzi mkuu 2020 uliopelekea wanachama tisa kujiondoa kwenye harakati za kutafuta Uhuru, haki na maendeleo ya watu nakuingia bungeni kinyume na sheria pamoja na Katiba ya nchi.

Kesho Mhe. Mbowe atazungumza na vyombo vya habari, nyuma ya hotuba yake lipo deni lakusimamia uhuru, haki na maendeleo ya watu ikiwa ni kauli mbiu waliyotumia kuwaomba wananchi kura. Wananchi waliwapa kura ila watawala hawakutaka kura za wananchi zihesabiwe bali wao wateue watu wanaodhani wanafaa.

Lakini pia ipo agenda ya Katiba mpya ambayo kila mtanzania msomi na asiyesoma anaelewa fika ndiyo nguzo yakutuvusha Kama taifa. Huu siyo msimamo au agenda ya viongozi wa CCM ila ni agenda ya upinzani, wanaharakati na wananchi wanaoitakia mema nchi yao. Mhe. Mbowe ataweza kuja na mbinu zakufikisha agenda hii mbele bila kuingia kwenye meza ya mazungumzo na watesi wetu CCM?

Hipo hoja ya kuwa na chama Cha siasa kisichokubali kwa namna yoyote kushirikiana na chama dola isipokuwa kwa agenda zenye maslahi ya Taifa letu. Je, Mhe. Mbowe anaweza kutuakikishia hiyo kesho kwamba wanachama na wapenzi wa chadema wapo tayari kuishi kwa njaa lakini wasimamie kupatikana haki, Uhuru na maendeleo ya watu?

Tunayo tume ya uchaguzi ambayo kimantiki ni wateule wa Rais aliyepo na ambayo kimantiki si tume huru ya uchaguzi ila ni tume ya uchaguzi kwa maana ya kikosi Cha watu wenye vyeo, je anatuakikishia kwamba chadema watasusia chaguzi zote Hadi tuwe na time huru?

Mwisho Kuna watu wameibuka na kauli tata, jana walituaminisha hivi leo wanatuaminisha vile. Watu hawa ni wasomi ila kimantiki hawana akili, je anashauri tutumie mbinu gani kukabiliana na njama za kundi hili lakisiasa linaloangalia maslahi?
FB_IMG_1589397986327.jpg
 
KWANI MBOWE HAJAFA??
SINILISIKIA KUWA KAKATA MOTO HUKO MAMBELEEE.....!

mimi napita tu jamani niko na familiya
[emoji848][emoji848][emoji848]
IMG-20210409-WA0008.jpg
 
Nampongeza Mhe. Mbowe, ameongea kitaalamu, ameongea kwa hoja nakuibua mjadala wa kitaifa. Ameeleza kiundani umuhimu wakuliponya Taifa, amesema katiba siyo hisani ya mtu, amedai haki kwa kila mmoja ameeleza vizuri namna alivyomkubali JPM kwa udhubutu na maamuzi magumu.

Huyu ni mwanasiasa lakini pia nikiongozi anayejipa muda wakutafakari kabla yakusema. Tukizungumza kwa upana huu naiona Tanzania mpya yenye watu making.

Naamini wapo vijana wanatamani wawe Kama Mbowe na prof Assad

Beatrice hongera kwakuweka dira katika hoja hii nadhani umemsaidia mwenyekiti kuweka sawa baadhi ya mambo hasa wafuasi wake walipoona thread hii, wahaya mmeanza kuona mbaya
 
Back
Top Bottom