Je, gari yako inatetemeka, engine kumisi au ukiwasha inazima inapokuwa ya baridi?

Usije kuwa uliweka mafuta mabaya...

Hiyo violent R.P.M ni ikiwa silent au hata ukiwa unaendesha?

Violent nikiwa naendesha, uendeshaji wangu nikiwa chini ya 100km/h huwa naendesha gari chini ya 2000 RPM na huwa najitahidi niendeshee hapo kwa maana huwa naacha RPM na engine ipokee taratibu bila kuiforce kufanya kazi.

Lakini kwa sasa naweza kuwa speed ya 50km/h ama 60 but RPM unakuta ipo 2500 huko ilhali nakuwa sijakanyaga sana mafuta na baada ya muda inarudi katika normal baada ya gia kujibadilisha. Plus ikiwa katika motion, unaweza shangaa RPM imetoka ghafla 2000 mpaka 2500 na kurudi 1800 then inarudi 2000.
 

Hilo la kushtuka ukiweka D kama ATF iko kwenye level inayotakiwa na haijachoka basi shida ipo kwenye Torque conveter, na mfumo wake wa umeme kiujumla(solenoid, wires n.k.)

Kuchelewa kubadili gear sijui inachelewa kubadili gear namba ngapi?
 

Kama hilo tatizo la rpm kubadilikabadilika linakukuta mara kwa mara basi Throttle Position Sensor ni kimeo.

Ila kama linakuja na kupotea basi wasiwasi wangu utakuwa kwenye mafuta yenyewe au kuna pressure ndogo kwenye njia ya mafuta...
 
Same to me kwenye Carina,kwangu mimi ilifika wakati ili gari liwake ni lazima nitumie combination ya ignition switch na accelerator kwa wakati mmoja,na gari likiwa idle ni lazima nijitahd kuhakikisha RPM haishuki 1by pressing accelerator pedal sababu usipo balance pedal RPM inashuka 0 na gari huzima.

Nilijaribu kupandisha silence still haikusaidia,then kuna Fundi akanisaidia kuondoa hiyo changamoto just by applying greaser kwenye ki valve ambacho kipo sehemu ya intake ya hewa ambacho kutokana na umri wa gari kilikwama.
 
Umekagua fuel pressure regulator na transmission fluid ya gari lako..?
 

IACV hiyo ndio ilikuwa inapelekea hiyo shida...

Ikikwama huku imefungua sana sailensa inakuwa juu na ukishusha haishuki.

Ikikwama huku imefungua kidogo basi ndo itakuwa inazima kila ukiwasha...
 
Kuna gari ina blink OD light na ikifanya hivyo gari huwa ina sleep mno na kukosa nguvu. Nimeifanyia diagnosis several times hakuna cha maana.
Control box imebadilishwa na zile Speed sensor ila bado ishu iko palepale.
Ushauri tafadhali..!
 
Kuna gari ina blink OD light na ikifanya hivyo gari huwa ina sleep mno na kukosa nguvu. Nimeifanyia diagnosis several times hakuna cha maana.
Control box imebadilishwa na zile Speed sensor ila bado ishu iko palepale.
Ushauri tafadhali..!

Gari aina gani na model ya mwaka gani?

Hiyo diagnosis uliyofanya ni ya Gearbox?

Kuna uwezekano valve body imejaa uchafu. Nijibu kwanza hayo maswali hapo juu.
 
hio Miss yako inasababishwa na hio Oxygen sensor. Hio ni sensor inayokaa kwenye Cat converter. Nimeona umesema una Mark X which is V6, kama unaweza kupata chart ya kujua firing order ya hio engine, upande wenye cylinder no. 1 ni Bank 1 na upande mwengine ndio Bank 2
 
Leak ya oil ama hewa.? How about plug.? Nyiongeza, gari ilikuwa parked bila kuwashwa kwa kama siku 5 hivi. Siku nimekuja kuiwasha, single switch haikutosha kuiwasha...
Angalia,isije kuwa watu wamekula madini ya kwenye exhaust humo. Mafundi wa mjini na wajinga wachache wana tabia hiyo sana.

Kaguo kuona kama makinikia yapo
 
Inawezekana gearbox oil imekwisha nguvu yake. Waone mafundi waikague.

Hope gari yako ni 4WD, kama ndio hako kamshindo ni kawaida hasa kama bush na mounting haziko vizuri
 
Mkuu habari nashukuru sana kwa kuoa huu uzi wako.

Nina volkswagen polo ya 2006.. ina tatizo moja linafanana na uzi wako.

Napata shida kuliwasha asubuhi (au likiwa la baridi) naweza ku attempt mara kadhaa ndio inawaka... then inakua haina power kabisa so nakanyaga acceleration mpaka baada ya sekunde kadhaa ndio inapata power then inakua na nguvu kama kawaida. Au nkiwasha nakanyaga resi haraka ili isizime... Baada ya hapo haisumbui kuwaka tena mpaka asubuhi ikiwa ya baridi. Pia taa ya check engine ipo ON mda wote

Kuna fundi mmoja aliniambia tatizo ni oxygen sensor.. naomba kujua kwa utaalamu wako shida ni nini?

asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…