Je, gari yenye engine capacity chini ya cc 1000 inafaa kwa safari ndefu?

Safari ndefu unamaanisha kutoka tz hadi south africa au mbagala to bunju au dar to moro au ubingo to mwenge?
 
Gari yenye cc chini ya 1000???
Hiyo ni pikipiki sasa....
 
Huwezi kusafiri safari ya Dar Bukoba moja kwa moja. Lazima usimame sehemu ujisaidie, ule chakula, uongeze wese na kujinyoosha pia. Inayoenda moja kwa moja ni ndege tu. Kwa ufupi Vits ya cc 990 inaweza toka South Africa mpaka Dar kama gari nyingine tatizo ni nguvu tu ya engine utakuwa unapigwa overtake mpaka na wakimbia Marathon
 
[emoji1787][emoji1787] hadi wakimbia marathoni??
 
Sio kweli tembeza chuma hata kwenda ahera angalia tu taa ya joto isipo waka gari ipo salama. Zingatia service
 
Hata kuitembeza kila siku inaweza kikubwa ni service kikiharibika kitu unafanya service fasta
 
Toyota succeed/probox ina tofauti gani na IST kwa upande wa injini?
 
Kufika unafika lakini njiani usijaribu kujipima ubavu na kina kluger, crown, subaru, prado n.k. Ukiwaona kwenye rear view mirror au side mirror waache wapite kwa amani na safari yako itakuwa poa.
Prado gani mkuu maana zipo za aina nyingi,mfano yenye injini ya 5L inapitwa hata na passo muungurumo mkubwa mwendo mdogo kwa hiyo jaribu kutoa specs ya gari husika.
 
Prado gani mkuu maana zipo za aina nyingi,mfano yenye injini ya 5L inapitwa hata na passo muungurumo mkubwa mwendo mdogo kwa hiyo jaribu kutoa specs ya gari husika.
Zile j150, zinakuwaga na kamluzi amazing ka turbo
 
Mimi sina gari mkuu, ila maisha mitandaoni, kwa vile hatuonani, kila mtu anajiona yuko zaidi, kumbe wengi hata pa kulala tunavizia, ila tunamiliki Simu ya kupondea vitu vya watu tu.

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Vip subaru engine yake iko vip kama unaisafiria Sana mkoan kwa mwezi unatembea klm 800 apo ikoje
#subaru impreza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…