Kama pikipiki tena yenye air-cooler inaenda itashindwaje gari yenye rejeta?
Sema kama alivosema mdau
Mwl.RCT hapo juu, ushajua gari yangu haiwezi shindana na wenye 2.0L zingatia haya:
1. Take it slow. Kama unahitajika uko "masafa marefu" mapema ni bora ukaondoka siku moja kabla kuliko kukimbizana njiani.
2. Jiwekee vituo kadhaa. Mfano kila baada ya 80-100km au 2 hours of driving itategemea pana mji au centre pumzika. Simamisha gari. Pata msosi afu zunguka zunguka ufanye utalii.
3. Ifanyie service kabla haujaondoka. Especially ya Oil, matairi, breki, etc.
4. Usibebe mizigo kupiliza. Ushajua gari yako haina cc kubwa so na nguvu (hp) itakua ndogo, usijibebee mizigo utaitesa. Mfano ukataka ule vichwa njiani lets say 3, pia ukabeba na mazawadi mazawadi unaweza ona una save kumbe unalitesa gari.
5. Mkiwa wawili itakua poa. Kupokezana maana hiyo safari ni ndefu.
6. Obey sheria zote ili kupunguza gharama za kuwatoa toa trafick.
Kwa experience yangu mimi nishaenda na IST Mbeya na Dodoma nishaipeleka Passo kwa mteja.