Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Nilikuwa napitia mtandao wa wikipedia, ili kusoma historia ya vita vya Kagera, tahamaki nikakuta webpage moja wanalichambua jeshi la wananchi wa Tanzania kinaga ubaga, nikashituka sana, je hizi habari hazihatarishi usalama wa Taifa?. hebu cheki hii link hapa
Tanzania People's Defence Force - Wikipedia, the free encyclopedia
Gamba la Nyoka mkuu heshima mbele. Ninavyoelewa mimi taarifa zilizoandikwa hapo haziwezi kuhatarisha usalama wa Taifa kwani hakuna kitu sisi tunachokiiti siri ambacho hakifahamiki na wazungu kwani silaha zenyewe tunanunua kwao halafu kwa umaskini wetu World Bank na IMF huwa wanadodosa juu yA MILITARY SPENDING YETU KABLA HAWAJATUFADHILI MIKOPO; tunalazimika kuwapa taarifa za majeshi yetu!! Taarifa za jeshi letu sio siri tena na ndio maana hata wewe umeweza kuzipata!!! Usalama wa Taifa letu ni jukumu letu mimi na wewe kuwatokomeza hawa mafisadi kwani fisadi kama Rostam anaweza kuliangamiza Taifa letu kwa jinsi alivyowaweka mifukoni viongozi wa nchi yetu!!
CIA facts file zooote wanazo wala tusijidanganye....wanajua uwezo wetu na wanajua tuna silaha kiasi gani na uwezo gani...jamaa wanajua hata linimabomu yetu yata expire na ziko tani ngapi....sisi tunajua kupiga domo siasa za kinafiki hatuna strategy yeyote......
Siku hizi hao wazungu nao wameshaingia mpaka jeshini... nimeshawaona kadhaa wakiwa wanarandaranda na magari ya jeshi. nadhani ukiuliza utaambiwa ni washauri, kama wale waliopo pale wizara ya fedha
We acha tu!Sasa ole wake habari hii ingeandikwa kwenye magazeti yetu ya nyumbani !! mwandishi, mmiliki, ndugu na jamaa zake, wangepotea mara moja....
Nakubaliana kuwa hazihatarishi,yale mambo ya siri ya jeshi ni zamani,kwenye dunia ya sasa everything is out in the open,kwa mfano rais wa marekani huwa anakuwa briefed kuhusu viongozi wote wanaowa consider kuwa ni maadui wa marekani,nyendo zao zote,maisha yao ya kila siku na mpaka wanapolala, wanachokula,kama wanaumwa ni ugonjwa gani nk...Saddam nae walikuwa wakimfuatilia hivyo hivyo sema alikuwa akibadilisha magari na kujidai amelala kwenye ikulu hii na kumbe keshaondoka na gari nyingine unsuspected,matokeo yake wakipiga bomu wanakuta hola...Ila cha muhimu ni kwamba alikuwa tracked.Kwa utaratibu huu wa satelite nk utaficha nini? Kwanza silaha tunazouziwa wanachagua wao zipi watuuzie na zipi wasituuzie,na rekodi zote wanazo za kila aina ya silaha wanazotuuzia....Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu,hakuna nchi zinazokwenda vitani na hazijui capabilities za mpinzani wake,Alkaeda wenyewe wanajulikana uwezo wao ndio iwe serikali? Kuna majasusi ambao kazi yao ni kusnoop tu,Korea Kaskazini wanajulikana uwezo wao,China,Japan nk...Sasa sisi tunadhani kuwa tukinunua kwa Mrusi ama Mchina basi nobody will know,tunajidanganya ama tulikuwa tukijidanganya kwasababu kuna watu ambao kazi yao ni ku constantly update hizo info,zote wanazo kwenye databases zao,tena current na sio hizo za Wikipedia ambazo mtu yoyote anaweza kuja kuzibadilisha kuzimanipulate.hazihatarishi
marekani wanajua idadi ya russia ana mizinga ya nuclear mingapi na russia anajua marekani ana nuclear ngapi...........
duniani hamna siri...