Je habari hizi hazihatarishi usalama wa taifa?

Je habari hizi hazihatarishi usalama wa taifa?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Posts
7,036
Reaction score
9,331
Nilikuwa napitia mtandao wa wikipedia, ili kusoma historia ya vita vya Kagera, tahamaki nikakuta webpage moja wanalichambua jeshi la wananchi wa Tanzania kinaga ubaga, nikashituka sana, je hizi habari hazihatarishi usalama wa Taifa?.

i344_WikiPedia1.jpg

i345_WikiPedia2.jpg

i346_WikiPedia3.jpg

i347_WikiPedia4.jpg

i348_WikiPedia5.jpg

i349_WikiPedia6.jpg

hebu cheki hii link hapa

[ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Military_of_Tanzania"]Tanzania People's Defence Force - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]
 
Nilikuwa napitia mtandao wa wikipedia, ili kusoma historia ya vita vya Kagera, tahamaki nikakuta webpage moja wanalichambua jeshi la wananchi wa Tanzania kinaga ubaga, nikashituka sana, je hizi habari hazihatarishi usalama wa Taifa?. hebu cheki hii link hapa
Tanzania People's Defence Force - Wikipedia, the free encyclopedia

Gamba la Nyoka, nimeisoma habari hiyo. Nivizuri hii linki wakaipata wahusika ili wajilidhishe kama haina madhara kuwekwa kwenye mtandao.
 
Duh! hii ni Hatarishi kabisa maana wamechambua kweli vifaa vilivyomo kwa jeshi letu..haya ndo matatizo ya utandawazi mambo ya ndani ya nchi yanawekwa wazi tu ..
 
Gamba la Nyoka mkuu heshima mbele. Ninavyoelewa mimi taarifa zilizoandikwa hapo haziwezi kuhatarisha usalama wa Taifa kwani hakuna kitu sisi tunachokiiti siri ambacho hakifahamiki na wazungu kwani silaha zenyewe tunanunua kwao halafu kwa umaskini wetu World Bank na IMF huwa wanadodosa juu yA MILITARY SPENDING YETU KABLA HAWAJATUFADHILI MIKOPO; tunalazimika kuwapa taarifa za majeshi yetu!! Taarifa za jeshi letu sio siri tena na ndio maana hata wewe umeweza kuzipata!!! Usalama wa Taifa letu ni jukumu letu mimi na wewe kuwatokomeza hawa mafisadi kwani fisadi kama Rostam anaweza kuliangamiza Taifa letu kwa jinsi alivyowaweka mifukoni viongozi wa nchi yetu!!
 
Strongly supporting you. Usalama wa Taifa letu unahatarishwa na mafisadi.
 
Hatuna siri in short.. kala ka bunker feki pale lugalo is probably all we gat..lol
 
Siku hizi hao wazungu nao wameshaingia mpaka jeshini... nimeshawaona kadhaa wakiwa wanarandaranda na magari ya jeshi. nadhani ukiuliza utaambiwa ni washauri, kama wale waliopo pale wizara ya fedha
 
si hayo tu kwani hata ukipitia baadhi ya dossiers za cia wanaonyesha kila nchi na uwezo iliokuw nao katika medani ya ulinzi ukweli hakuna cha kujificha ikiwa india na pakisatani walianza kufanya siri majaribio ya makombora, wakubwa wakapata habari kabla ya hata jaribio la mwanzo kufanywa itakuwa sisi tuso mbele wala nyuma, kila kitu chetu kiko uchi.
 
CIA facts file zooote wanazo wala tusijidanganye....wanajua uwezo wetu na wanajua tuna silaha kiasi gani na uwezo gani...jamaa wanajua hata linimabomu yetu yata expire na ziko tani ngapi....sisi tunajua kupiga domo siasa za kinafiki hatuna strategy yeyote......
 
true ...kila nchi duniani mambo yapo wazi sana siku hizi...habari kama hizi kabla ya maendeleo ya teknelojia ingetakiwa kazi ya miaka ..ili kuweza kupata information kama hizi za maadui....
 
Siku hizi hao wazungu nao wameshaingia mpaka jeshini... nimeshawaona kadhaa wakiwa wanarandaranda na magari ya jeshi. nadhani ukiuliza utaambiwa ni washauri, kama wale waliopo pale wizara ya fedha

Ni 'washauri' toka Marekani na wameingia kwa wingi wakati wa Kichaka kutokana na 'urafiki wake wa karibu' na Mkuu wa nchi.
 
Msibabaike na hayo kwani ni mambu ya kawaida kabisa na data hizo huwa zinapatikana katika kila nchi,ila ni jambo moja ambalo wahusika wa mambo ya kijeshi hawayaamini kabisa unaweza kusema hicho ni kivuli cha Tanzania lakini kama kilivyo kivuli huwezi kujua kuwa kina kovu au jicho moja halioni au macho yote mawili hayaoni ,silaha kila siku zinakuwa upgrade na ndege za kivita pia ,sasa unaamini kuwa tutatumia ndege za kivita zilizo tengenezwa miaka selasini iliyopita hivi tunaenda kupigana na kunguru ,maana dunia ya leo ukipeleka ndege hizo hakikisha hairudi hata moja ,maana kuna Sukoi na F 16 hazina mchezo ,ila katika hiyo habari kuna kaukweli fulani kuwa hatuna mapilot wanaoweza kumanuva harakati za angani ,tunahitaji kuwapeleka mapilot wetu Pakistani huko kuna watu ni wakorofi kwa machezo ya angani inasemekana kuliko nchi nyengine yeyote.
Ila kuna ndege za kivita zetu WaZanzibari ,WaTanganyika mlizichukua bila ya rizaa.True story. 😀
 
Pamoja na kuwa uwezo wetu kijeshi waweza kujulikana........lakini don't rely on Wikipedia
 
Habari hizo si hatari kwa usalama wa Taifa kwa sababu zimetolewa ndani ya Jeshi zikiwa 'Ndivyo Sivyo' ili umma na jumuiya ya kimataifa uelewe hivyo.

Data hizo ni za mwaka 47.

Kujua nchi ina nini, sio hatari kwa usalama, bali hatari kwa usalama ni kujua nini kiko wapi. Data zimesema tuu tuna nini lakini hakuna data nini kiko wapi.

Kujua Lugalo ni kambi ya Jeshi, ni public information. Kujua ndani ya Lugalo nini kiko wapi ndio classified information.
 
Sasa ole wake habari hii ingeandikwa kwenye magazeti yetu ya nyumbani !! mwandishi, mmiliki, ndugu na jamaa zake, wangepotea mara moja....
 
hazihatarishi
marekani wanajua idadi ya russia ana mizinga ya nuclear mingapi na russia anajua marekani ana nuclear ngapi...........
duniani hamna siri...
 
hazihatarishi
marekani wanajua idadi ya russia ana mizinga ya nuclear mingapi na russia anajua marekani ana nuclear ngapi...........
duniani hamna siri...
Nakubaliana kuwa hazihatarishi,yale mambo ya siri ya jeshi ni zamani,kwenye dunia ya sasa everything is out in the open,kwa mfano rais wa marekani huwa anakuwa briefed kuhusu viongozi wote wanaowa consider kuwa ni maadui wa marekani,nyendo zao zote,maisha yao ya kila siku na mpaka wanapolala, wanachokula,kama wanaumwa ni ugonjwa gani nk...Saddam nae walikuwa wakimfuatilia hivyo hivyo sema alikuwa akibadilisha magari na kujidai amelala kwenye ikulu hii na kumbe keshaondoka na gari nyingine unsuspected,matokeo yake wakipiga bomu wanakuta hola...Ila cha muhimu ni kwamba alikuwa tracked.Kwa utaratibu huu wa satelite nk utaficha nini? Kwanza silaha tunazouziwa wanachagua wao zipi watuuzie na zipi wasituuzie,na rekodi zote wanazo za kila aina ya silaha wanazotuuzia....Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu,hakuna nchi zinazokwenda vitani na hazijui capabilities za mpinzani wake,Alkaeda wenyewe wanajulikana uwezo wao ndio iwe serikali? Kuna majasusi ambao kazi yao ni kusnoop tu,Korea Kaskazini wanajulikana uwezo wao,China,Japan nk...Sasa sisi tunadhani kuwa tukinunua kwa Mrusi ama Mchina basi nobody will know,tunajidanganya ama tulikuwa tukijidanganya kwasababu kuna watu ambao kazi yao ni ku constantly update hizo info,zote wanazo kwenye databases zao,tena current na sio hizo za Wikipedia ambazo mtu yoyote anaweza kuja kuzibadilisha kuzimanipulate.
 
Back
Top Bottom