KERO Je hakuna namna ya kuwadhibiti madalali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
mkimaliza huko twende kariakoo, haiwezekani nishafika dukani na mwenye duka hatambuliki ni nani unaishia kuzungukwa na watu wawili watatu, hii kamisheni ya namna gani wakati nishafika dukani?
mkimaliza huko twende kariakoo, haiwezekani nishafika dukani na mwenye duka hatambuliki ni nani unaishia kuzungukwa na watu wawili watatu, hii kamisheni ya namna gani wakati nishafika dukani?
Hawa wanajiita mawinga
 
Mmezidi bana😂
Mmeamua kutusimanga madalali si ndiyo? Kila mtu ashinde mechi zake za nyumbani tusichunguzane alafu nilihama kwenye uwinga baada ya humu kusimangwa mmekuja tena kwenye udalali daaaaah
 
Zamani kidogo kulikuwa na madalali wenye ofisi. Walikuwa wana leseni na wanalipa kodi.

Mwenye kitu cha kuuza anakabidhi kwa dalali kwa makubaliano ya asilimia ya kamisheni.

Siku hizi imekuwa shughuli holela inayoondosha hata usalama wa mnunuzi. Dalali hana kituo cha kazi.
 

Ni washenzi kweli kweli unakuta mwenyenacho anauhitaji wa pesa ya haraka wao wanakikwamisha kwa kuongeza bei kubwa
 
Imagine sasa hivi Dodoma kiwanja tu tena ndani ndani huko hakuna umeme wala barabara lakini kinauzwa bei ghari kuliko IST
 
Makubaliano yaliyo nje ya scope ya sheria husika ni batili.
Kuna kitu hujakielewa bado yaani iko hivi dalali amekupeleka kwenye kiwanja kisha amekupa bei ukileta ulalamishi anakwambia basi kama huwezi nenda sijakulazimisha atakuja anayemudu hapo utakuwa umekikosa kiwanja maana hauna connection na mmiliki wa kiwanja
 
Ndiyo maana kuna jamaa katoa hint kwamba heri umsake mmiliki mwenyewe...ukiamua kum spy mmiliki halali unampata kama una time na uvumilivu...

Madalali ni matapeli tu..
 
Ndiyo maana kuna jamaa katoa hint kwamba heri umsake mmiliki mwenyewe...ukiamua kum spy mmiliki halali unampata kama una time na uvumilivu...

Madalali ni matapeli tu..
Kumpata mmiliki halali itakucost muda badala ya kutumia wiki moja itakugharimu miezi 3 au 6 ili upate na kumbuka hao wamiliki wanakuwa na uhusiano wa kibishara na madalali na hawataki kusalitiana wanawekeana viapo vya kutozungukana ukiwafuata wewe wanaficha
 
Ni washenzi kweli kweli unakuta mwenyenacho anauhitaji wa pesa ya haraka wao wanakikwamisha kwa kuongeza bei kubwa
Kwani wanaweka zuio kwamba mwenye mali haruhusiwi kuendelea wateja? If not, usiwalaumu; tafuta wateja na wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…