Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Internship zingine watu hawalipwi kabisa. Unatumia hela yako kwenye nauli na chakula. Yaani hata jero hupewiIntern ni namna ya kuwatafutia ulaji hao graduates ambao hawana kazi za kufanya , wakitaka ajira lazima wafuate mlolongo mreeefu...
Sio nusu, ni wengi wao hawajachaguliwa kupata kazi.Hili ni wazo zuri litafutiwe ufumbuzi. Rais Samia alitoa ajira mpya kada ya elimu cha kushangaza na huzuni walimu walokuwa wanajitolea nusu hawakuchaguliwa
Upo sahihi mkuu. Maana unachoma nauli na kuingia gharama bure bila kufaidika lolote.Ni ufala sana ku volunteer bure bora nikae nyumbani
Yaani wanakupa moyo balaa. Ukisepa tu hawakutafuti na inapita hata miaka mitano 🤣. Halafu wiki inayofuata baada ya kumaliza internship unaona wanatangaza wanahitaji interns wengine.Siri kuu ya hii kitu ni hii :- kampuni huwa ipo behind na productions sasa inahitaji nguvu kazi, ili kukamilisha order walionayo. Kuajiri temp inakuwa ngumu hawa lazima walipwe ujira wao. Kwahio njia ya kutumia ndio hii intern na volunteer(utumwa mambo leo wa ajira). Unafanya kazi kwa bidii ukijua utapata ajira kumbe manager/supervisor/group leader na HR wanakucheka tu. Manake wakisha keep up na production yao ndio wanakwambia nenda nyumbani zaidi tutakupigia hapo kimya cha milele kimefika.
Yaani makampuni mengi sana, mashirika mengi sana, mashirika/taasisi za kiserikali, halmashauri na NGO kama zote wao wanataka maintern na volunteer tu.Nawaambia vijana acheni ujinga, narudia acheni ujinga na hayo ma interns sijui volunteer, mnaharibu.
Mtoa mada kasema la ukweli na mjue kuwa hayo makampuni yanaepuka mapato na malipo mengi sana kwa sababu yenu, moja wengi kwa sasa hawatoi ajira wanaendesha makampuni, mahoteli nk kwa mfumo huo.
Ndiyo maana wanakuja kuchuma hapa bongo kwa mawazo ya akili zenu za kufanya kazi bure, tuna mifano hai hoteli, kampuni zinabadirisha staff kila uchao, ukiuliza unaambiwa wamemaliza muda na wanaingia wengine.
Vijana mnabemendwa kwa ujinga wenu, shitukeni.
Hii kitu ni utumwa na unyonyaji. Sehemu zingine mtu hupewi hata elfu moja ya maji.Kiukweli huu ni unyonyaji ,kuna watu wana jitolea had mwaka na nusu, had unajiuliza kama wanaitaj man power kwanini wasiajir hata temporary contracts za mwaka Moja moja,
Wanakudanganya na elfu 40 ,zao za weekly, haki mim bora niuze genge langu
Mashirika ya serikali, taasisi, NGO, makampuni binafsi mengi sana yanayo watu wengi mno wa kujitolea. Mpaka hawa wawekezaji wanaokuja kuwekeza Tanzania na wenyewe wamesomba ma intern, volunteer wa kutosha.Hata RUWASA wanao vijana wa kujitolea lakini hakuna chochote na wanaajiri wengine tu.
mtu anawezaje kufika mbele bila kuwa na mtu kule wala kuattend masomo?Intern ni namna ya kuwatafutia ulaji hao graduates ambao hawana kazi za kufanya , wakitaka ajira lazima wafuate mlolongo mreeefu sasa short cut wanawaita intern huku wanawalipa vijihela vya kuishi sihaba kuliko kukaa tu nyumbani maana elimu yetu imejikita katika kuajiriwa tu . wachache tulioshtuka tukaamua kuja kubeba boksi huku ndio tunasonga kwa namna hii.
Ndio njia pekee ya kujudge competence ya mwajiriwa kabla hujamwajiri kwa kuangalia vyetiSiku hizi kumeibuka tabia ya mashirika na makampuni binafsi na ya serikali kupenda ma intern/volunteer/wa kujitolea kwa sana.
Je, ni jambo jema? Wengine hawalipwi kabisa, wengine wanalipwa kidogo. Pia wanatoa ahadi hewa za kukupa ujuzi au kukupa mkataba ambao hautaupata bila connection.
NB: Leo kuna mlevi mmoja aliropoka "Nyie mnaojitolea mkipata ajira au mkataba niiteni mbwa, nimekaa paleee."