Je hali ya uchumi wa nchi kwa sasa inaakisi uboreshaji wa maisha kwa wananchi wake?

Je hali ya uchumi wa nchi kwa sasa inaakisi uboreshaji wa maisha kwa wananchi wake?

Nuel27

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2026
Posts
461
Reaction score
915
Anaandika mwandishi na mchambuzi wa Clouds Media Group Farhan Kihamu

ORODHA YA MASWALI YANGU KWA MBUNGE WANGU AYAPELEKE BUNGENI KWA MAWAZIRI HUSIKA.

1- Mheshimiwa Mbunge suala la sekta Ardhi na Makazi naomba ufikishe kwa Waziri wa Ardhi kuwa kitaani kwasasa haswa Mijini Chumba, sebule, jiko na choo ni zaidi ya 400,000 kwa mwezi maana yake Watanzania wanatafuta pesa kwa ajili ya usingizi pekee?

2- Mbunge wangu shika karatasi ukifika Bungeni simama tena ulizia kuhusu sekta ya ardhi tunaenda wapi? Ardhi imepanda bei kuliko kawaida, Watanzania wananunua ardhi kwa bei ya juu inakimbizana na Ujenzi, miradi ikitangazwa haichukui sekunde imekata, je tuna gap kubwa la walionazo na wasio nazo?

3- Swali la nyongeza litasalia bei ya soko kwenye ardhi na Makazi inapaa kuliko magari, nani atasimama kwa ajili ya Mama Ntilie? Miradi ya Mtanzania wa kawaida Machinga, Mama Ntilie ni lini ataweza kumiliki Nyumba na ardhi kwa kasi hii? Tunasogea wapi kama nchi kwenye sekta ya Real Estate?

4- Mheshimiwa Mbunge tafadhali usisahau kuingia kwenye Wizara ya Elimu kwasasa Ada zinazidi kupaa kwenye Private Schools ambacho tunaelewa, lakini nani angalau ajitokeze atoe bei elekezi na regulation ya ada kusaidia Wazazi? Lini tutapambana kuhakikisha shule zetu za Umma haswa msingi zijae Walimu na kutoa ushindani?

5- Mbunge wangu usisahau kugusia suala la AJIRA, nimeona Wageni wengi wanakuja nchini haswa kutoka Taifa lile kubwa la Asia ambacho tunapongeza lakini kama Mgeni anakuja kama Winga, Dalali na Mtu kati vipi kuhusu Mtanzania wa kawaida? Tumejiandaaje na wimbi hili kabla ya kufikia mambo ya Kusini mwa Africa? Mtanzania bado Ajira kilio lakini wapo wanakuja wanazidi kuziba mirija ya ajira tunaendaje?

6- Mheshimiwa Mbunge naomba la mwisho ukifika tuungane na aliyetaka Diamond ajengewe sanamu ila Wewe ongezea Majina ya Wasomi wakubwa wa nchi hii kama Erasto Mpemba wa MPEMBA EFFECT tujenge mfumo wa Wasomi kupata nafasi ya kuonana na Viongozi zaidi kuliko Wana wa mapambio zaidi ili wapate mawazo mapya.

7- MWISHO Msalimu sana Shomvi Abdallah Ulega Mwambie Wazaramo wanazidi kuondoka Dar Es Salaam pale Temeke inashushwa Bandari, wasisahau Dar sio biashara bali ni Makazi ya Watu na historia za harakati za Uhuru wa Tanganyika, tusisahau.

1789114746888.png
 
Back
Top Bottom